Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
1 4 2 /
M U N G U B A B A
Jiulize na kujijibu maswali yako mwenyewe kuhusu asili ya wema wa Mungu na ghadhabu yake. Tafakari mambo yako mwenyewe, na uangalie kama unayo maswali yoyote maalum yaliyosababishwa na kweli kuhusu wema wa Mungu na hasira yake dhidi ya uovu. Maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kuibua mawazo kadha wa kadha ndani yako mwenyewe! * Ikiwa Mungu ni mtakatifu kabisa, anawezaje kuwa na uhusiano wa aina yoyote na sisi au na uumbaji, ukizingatia kuwa sasa hivi sote tunaishi chini ya laana? * Ikiwa Mungu wetu ni Mungu wa upendo usio na mipaka, anawezaje kwa hakika kuacha hata nafsi moja kuangamia kuzimu? * Kwa kuwa damu ya Yesu imetuliza ghadhabu ya Mungu (yaani, ilitupatanisha na Baba) kwa nini watu wote hawaokolewi moja kwa moja hata bila kuomba msamaha? * Kwa kuzingatia ukweli kwamba Mungu ni mwenye neema na hashughuliki nasi kwa msingi wa sifa zetu bali kwa neema yake na upendo wake mkuu, kwa nini Mungu hajachagua kuokoa kila mtu kila mahali? Ikiwa Mungu hataki hata nafsi moja iangamie, kwa nini wanaangamia hata hivyo? * Je, unatatuaje na kuunganisha wazo la kwamba Mungu hunyesha mvua kwa wenye haki na wasio haki, wakati huo huo, hasira ya Mungu ni dhidi ya wale wanaopinga mapenzi yake na wokovu wake kwa njia ya Yesu Kristo? Hii inawezekanaje? * Inamaanisha nini kupokea neema ya Mungu bure? Je, inawezekana kwa mtu ambaye hapo awali alikuwa mrithi wa upendo na neema yake, kugeuka na kuwa mlengwa wa ghadhabu na hasira yake? Elezea jibu lako. Zungumzia na ueleze jinsi uhusiano wa Mungu na watu wake Israeli unavyoweza kutusaidia kuelewa asili ya upendo na haki ya Mungu kuhusiana na watu wake. Kwa mfano, watu wale wale ambao Mungu aliwaokoa kutoka katika utumwa na ukatili wa ukandamizaji wa Wamisri, walihukumiwa na Mungu kutangatanga kwa miaka arobaini nyikani kwa sababu ya kutokutii na kutokuamini kwao. Watu wale wale ambao waliokolewa na Mungu chini ya wafalme wa Israeli na Yuda walipelekwa uhamishoni chini ya falme mbili: Ashuru kwa ufalme wa Kaskazini, na Babeli kwa ufalme wa Kusini. Je, ni madokezo gani tunayoyapata kutokana na mfano wa Waisraeli kwamba upendo wa Mungu na haki yake vinatumika wakati mmoja katika kuhusiana kwake na watu wake? Watu wa Israeli
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
4
MIFANO
1
page 299 6
Made with FlippingBook - Share PDF online