Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 1 4 3

M U N G U B A B A

Hakuna Kuzimu?

Idadi kubwa ya makanisa ya kiinjili yanapitia upya fundisho la adhabu ya milele na kulifafanua upya katika msingi wa “maangamizo” badala ya “mateso yasiyokwisha mbali na uwepo wa Mungu milele.” Yakiwa yameguswa kwa kina na kuathiriwa na fundisho la Biblia juu ya upendo na wema wa Mungu Baba Mwenyezi, yanatazama tena kwa makini maandiko ambayo yanatumika katika kutetea dhana ya mahali ambapo wale wanaomkana Mungu watakuwa katika uchungu milele. Badala ya wazo kama hilo, wanasisitiza wazo la kwamba Mungu ataharibu au kuwaangamiza adui zake, lakini hatawaacha wakiendelea kuwa hai na wanajiotambua kwa kusudi la kuwatesa. Jadili mfano wa fundisho la kuzimu kama kielelezo cha hitaji la kanisa kugundua na kuelezea upya fundisho la kibiblia juu ya ghadhabu ya Mungu Baba Mwenyezi. Unazungumziaje majaribio haya ya kutafakari upya fundisho la kuzimu? Unakubaliana au hukubaliani nayo? Mwanatheolojia maarufu wa Kikatoloki (Karl Rahner) leo anajenga hoja ya kuelewa kifo cha Kristo kama wokovu wa ulimwengu wote. Katika mtazamo huu, kifo cha Kristo kinatumika kwa ujumla kwa mataifa yote na watu wote, na kwa maana hiyo familia zote na watu binafsi, iwe wanafahamu kazi ya Yesu msalabani au la. Kimsingi, hawa waliofunikwa na neema ya Mungu msalabani wanatambulika kama “Wakristo wasiojulikana,” wale ambao wamejumuishwa katika kazi ya wokovu ya Masihi Yesu msalabani, iwe wanaifahamu au la. Hakika, kuna maandiko katika Biblia ambayo yanaonekana kudokeza kwamba wokovu wa Mungu ni kwa watu wote kila mahali (rej. 1 Yoh. 2:1-2; 4:14; 5:19; Yoh. 1:29; 4:42; 11:51-52; 2 Kor. 5:18-21; Ufu. 12:9, nk). Je, mtu yeyote anaweza kutoa hoja halali kutoka kwenye Maandiko kwamba ulimwengu mzima umejumuishwa katika kielelezo cha wema wa Mungu katika Kristo – wote wataokolewa kutokana na kifo cha Yesu, au tu wale waliochaguliwa? Je, kuna tatizo gani (kama lipo) katika wazo la wokovu wa jumla kwa watu wote? Mungu huonyesha wema wake kupitia sifa zake za kiadili za usafi, uadilifu, ukamilifu, na upendo kamili usio na mipaka. Anaonyesha usafi wake kamili kupitia utakatifu, haki, na hukumu za haki. Anaonyesha uadilifu na ukamilifu wake kamili kupitia sifa za uhalisi, ukweli, na uaminifu. Hatimaye, Mungu anaonyesha upendo wake usio na mipaka kupitia sifa zake za ukarimu, neema, rehema, na ustahimilivu. Uelewa wa ghadhabu ya Mungu ni muhimu kwa picha sahihi ya kibiblia ya Mungu Baba Mwenyezi. Tunaelewa fundsho hili kuu la Maandiko tu tunapochunguza Wokovu wa Jumla kwa Wote

2

3

4

Marudio ya Tasnifu ya Somo

Made with FlippingBook - Share PDF online