Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
1 4 4 /
M U N G U B A B A
uhusiano kati ya wema wa Mungu na ukali wake. Hakuna mvutano uliopo kati ya upendo wa Mungu na ghadhabu yake, kwa kuwa ni Mungu mmoja wa kweli, daima anatenda kila mahali na katika mambo yote kwa uwiano na mwafaka kamili wa upendo na haki yake, neema na kweli.
Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo kuhusu wema wa Mungu Baba na ghadhabu yake, unaweza kuangalia vitabu vifuatavyo: Muncy, John. Whatever Happened to the Wrath of God? Library, PA: Ethnos Press, 1996. Yancey, Philip. What’s so Amazing about Grace? Grand Rapids: Zondervan, 2002. Sasa ni wakati wa kuhusianisha ufahamu ulioupata katika moduli hii na kazi yako ya Huduma kwa Vitendo, barua utakayokuwa ukiandika kwa rafiki halisi au wa kufikirika. Ili kutumia Maandiko ni lazima tuwe na ujuzi wa muktadha husika na hitaji tunalotafuta kushughulikia. Kazi hii mahususi imetengenezwa kwa ajili yako kufikiria kwa umakini namna unavyoweza kutumia kweli za moduli hii kwa mtu anayehitaji kusikia kwa ushawishi na kwa wazi habari njema za fursa ambayo Mungu ameitoa katika Yesu Kristo. Kufikia wakati huu, bila shaka umeweza kuangazia kwa kina maelezo ya kazi yako pamoja na Mkufunzi wako, na sasa ni wakati wako wa kutumia uelewa wako katika kazi hii. Kumbuka, lengo la masomo yote ni kukua katika namna ambayo itamruhusu kwanza kabisa Mungu, Roho Mtakatifu, kutumia kweli hizo maishani mwako, kisha atumie mafunzo haya kupitia wewe unapoandaa, kushauri, kufundisha, na kutia moyo wengine. Kazi hizi zimetengenezwa maalum ili kukusaidia kutumia kwa ustadi matunda ya Maandiko katika maisha na huduma yako. Unapofanya kazi hii, mwombe Bwana akupe uelewa unapoendelea kukamilisha kazi yako na kuwashirikisha wengine uelewa wako. Katika kipindi hiki cha mwisho, mwombe RohoMtakatifu auchunguze moyo wako na kukusaidia kutambua kama kuna watu, hali, au fursa zinazohitaji kufanyiwa maombezi kutokana na yale uliyojifunza katika somo hili au, kwa mapana zaidi, katika moduli hili. Msikilize Bwana kwa umakini hapa; Neno la Bwana daima huambatana na maongozi na misukumo ya Roho. Ni mambo gani au watu gani hasa wamekujia akilini kutokana na somo hili na wanahitaji dua na maombi
Nyenzo na Bibliographia
Kuhusianisha Somo na Huduma
4
Ushauri na Maombi
Made with FlippingBook - Share PDF online