Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 1 4 5

M U N G U B A B A

yako? Kuwa mtii kwa Bwana; chukua muda kutafakari hili, na kupokea usaidizi unaohitajika katika ushauri na maombi kwa yale ambayo Roho amekuonyesha.

MAZOEZI

Hakuna maandiko ya kukariri.

Kukariri Maandiko

Hakuna kazi ya kukabidhi.

Kazi ya Usomaji

Kufikia sasa, unapaswa kuwa umeainisha na kufanyia maamuzi mapendekezo yako kuhusiana na Kazi ya Huduma na Kazi ya Eksejesia na kuyakabidhi kwa Mkufunzi wako ili ayapitie na kuyapitisha rasmi. Hakuna vipindi zaidi vya moduli hii, kwa hiyo ni lazima uhakikishe kuwa umewasiliana na mwalimu wako, amekupa vigezo vyote na maelekezo muhimu kuhusu kazi zako, na kukubaliana juu ya tarehe ambayo utapaswa kukabidhi kazi zako. Mtihani wa mwisho utakuwa wa kwenda nao nyumbani, na utajumuisha maswali yaliyochukuliwa kutoka katika majaribio matatu ya kwanza, maswali mapya kutokana na maarifa yaliyofundishwa katika somo hili, na maswali ya insha ambayo yatahitaji majibu yako mafupi kwa maswali muhimu yenye lengo la kuhusianisha somo na huduma na maisha. Pia, wakati wa mtihani unapaswa kujiandaa kuandika au kutamka aya zilizokaririwa katika kozi hii. Ukimaliza mtihani wako, tafadhali mjulishe mkufunzi wako na uhakikishe kuwa anapata nakala yako. Tafadhali zingatia: Ufaulu wako katika moduli hii hauwezi kupimwa na kujulikana kama hautafanya mtihani wa mwisho na kukusanya kazi zote na kuzikabidhi kwa mkufunzi wako (Fomu ya Ripoti ya Usomaji, kazi za kihuduma, kazi za ufafanuzi wa Maandiko, na mtihani wa mwisho). Hakika hakuna njia ya kuelezea uzuri usio na kikomo, nguvu, na utukufu wa Mungu wetu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, au adhama ya nafsi ya kwanza ya Utatu, Mungu Baba Mwenyezi. Maneno ya Yesu kuhusu asili ya uzima wa milele yanagusa kiini chenyewe cha umuhimu wa kumjua Mungu na kutembea naye kwa imani katika Yesu, “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” Yoh. 17:3. Wokovu wetu unahusiana na ujuzi sahihi wa Mungu Baba Mwenyezi, na Mwanawe mpendwa Bwana wetu, Masihi Yesu.

Kazi Nyinginezo

page 299  7

Taarifa Kuhusu Mtihani wa Mwisho

4

Neno la Mwisho Kuhusu Moduli Hii

Made with FlippingBook - Share PDF online