Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

1 4 6 /

M U N G U B A B A

Matumaini yetu ya dhati ni kwamba Moduli hii itakuwa tu moja wapo ya hatua za kwanza za kumtafuta Mungu wetu maishani. Kama Mungu aliye hai na Muumba wa vitu vyote, Yeye hutamani kutamaniwa, na anaweza kupatikana tu tunapojitoa kikamilifu katika kumtafuta. Maombi ya wana wa Kora na yawe maono yako binafsi ya dhati na kusudi la maisha: Zaburi 42:1-2 – Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Ukuu na wema wa Mungu Baba Mwenyezi uyajaze maisha yako kwa maono na nguvu, ili uweze kumwakilisha Bwana kwa heshima kama mfuasi wake katika wakati na majira kama haya!

4

Made with FlippingBook - Share PDF online