Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 1 6 3

M U N G U B A B A

K I A M B A T I S H O C H A 1 3 Mapokeo (Paradosis) Mch. Dkt. Don L. Davis na Mch. Terry G. Cornett

Ufafanuzi wa Strong

Paradosis. Kuambukiza yaani (kihalisia) agizo; hususani, sheria ya mila ya kiyahudi.

Maelezo ya kamusi Vine’s Dictionary

Inaashiria “Mapokeo”, Na hivyo, kwa maneno mbadala, (a) “mafundisho ya rabi,” . . . (b) “mafundisho ya kitume,” . . . ya maagizo kuhusiana na mikusanyiko ya waamini, ya mafundisho ya Kikristo kwa ujumla . . . ya maelekezo kuhusu mwenendo wa kila siku.

1. Dhana ya mapokeo katika Maandiko kimsingi ni chanya.

Yeremia 6.16 - “Bwana asema hivi, simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, iko wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, hatutaki kwenda katika njia hiyo.’’ (ling. Kut. 3.15; Amu. 2.17; 1 Wafalme 8.57-58; Zab. 78.1-6). 2 Mambo ya Nyakati 35.25 “Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote waume kwa wake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hata leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika maombolezo.” (ling. Mwa. 32.32; Amu. 11.38-40). Yeremia 35.14-19 “Maneno ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru wanawe, kwamba wasinywe divai, yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana waitii hiyo amri ya baba yao; lakini mimi nimesema nanyi, nikiamka mapema na kunena, bali ninyi hamkunisikiliza mimi. 15 Pia naliwapeleka watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiamka mapema na kuwapeleka, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiwafuate miungu mingine, ili kuwatumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza. 16 Basi, kwa kuwa wana wa Yonadabu, mwana wa Rekabu, wameitimiza amri ya baba yao aliyowaamuru, lakini watu hawa hawakunisikiliza mimi; 17 kwa sababu hiyo,

Made with FlippingBook - Share PDF online