Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
1 6 4 /
M U N G U B A B A
Mapokeo (muendelezo)
asema BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli; Tazama nitaleta juu ya Yuda, na juu ya wenyeji wote wa Yerusalemu, mabaya yote niliyoyatamka juu yao; kwa sababu nimesema nao, wasinisikilize; nimewaita, wala hawakuniitikia. 18 Naye Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote, na kutenda sawasawa na yote aliyowaamuru; 19 basi, kwa sababu hiyo, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu, mwana wa Rekabu, hatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu hata milele. 2. Mapokeo ya kimungu ni kitu kizuri cha ajabu, lakini si mapokeo yote ni ya kimungu Kila mapokeo binafsi lazima yapimwe kulingana na namna yanavyohusiana na Neno la Mungu na manufaa yake katika kuwasaidia watu kutunza utii wao kwa kielelezo na mafundisho ya Kristo. 1 Katika Vitabu vya Injili, Yesu mara kwa mara anawakemea Mafarisayo kwa kushikilia mapokeo ambayo yanabatilisha amri za Mungu badala ya kuzihimiza. Marko 7.8 - “Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.” Wakolosai 2.8 - “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.” 3. Pasipo ujazo wa Roho Mtakatifu, na kuimarishwa kwetu kwa kudumu kwa njia ya Neno la Mungu, mapokeo bila shaka yatatuongoza kwenye taratibu mfu. Wale walio wa kiroho wamejazwa na Roho Mtakatifu, ambaye ni nguvu yake na uongozi wake pekee unaleta hali ya uhuru na uhai kwa mtu binafsi na kwa kusanyiko katika yote wanayo yatenda na kuyaamini. Hata hivyo, pale ambapo matendo na mafundisho ya mapokeo yoyote, hayaendelei kuvuviwa na nguvu za Roho Mtakatifu na Neno la Mungu, mapokeo hayo yanapoteza ufanisi wake na yanaweza kutokuwa na tija kwa ufuasi wetu katika Yesu Kristo.
1 “WWaprotestanti wote wanasisitiza kwamba mapokeo haya lazima yapimwe dhidi ya Maandiko na kamwe hayawezi kuchukua mamlaka huru ya kitume juu au sambamba na Maandiko.” (J. Van Engen, “Tradition,” Evangelical Dictionary of Theology , Walter Elwell, Gen. Ed.). Tungeongeza kwamba Maandiko yenyewe ndiyo “mapokeo yenye mamlaka” ambayo kwayo mapokeo mengine yote yanapimwa. Tazama,“Kiambatisho A, waanzilishi wa Mapokeo: Ngazi tatu za mamlaka ya kikristo, mwishoni mwa maelezo haya.
Made with FlippingBook - Share PDF online