Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 1 6 5

M U N G U B A B A

Mila (muendelezo)

Waefeso 5.18 - “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho” Wagalatia 5.22-25 - “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. 24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. 25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.” 2 Wakorintho 3.5-6 - “Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. 6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.” 4. Uaminifu kwa mapokeo ya kitume (mafundisho na kielelezo) ni chanzo cha ukomavu wa Kikristo. 2 Timotheo 2.2 - “Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.” 1 Wakorintho 11.1-2 - “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo 2 Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.” (linganisha. 1 Kor. 4.16-17, 2 Tim. 1.13-14, 2 the. 3.7-9, Fil. 4.9). 1 Wakorintho 15:3-8 – Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; 4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; 5 na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; 6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; 7 baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; 8 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.

Made with FlippingBook - Share PDF online