Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

1 7 2 /

M U N G U B A B A

Majina ya Mwenyezi Mungu (muendelezo)

3. Adonai linaweza kueleweka kumaanisha “Bwana wa wote ” au “Bwana aliye bora ” (rej. Kum. 10:17; Yos. 3:11). (Rej. Merrill F. Unger na William White, Jr., wahariri, Nelson’s Expository Dictionary of the Old Testament [Nashville: Nelson, 1980], uk. 228-29; na Otto Eissfeldt, “Adhon,” katika Theological Dictionary of the Old Testament, 1:59-72.) C. Yahweh (Yehova) 1. Jina Yahweh linatoa tafsiri ya tetragrammaton ya Kiebrania (neno lenye herufi nne) YHWH. Kwa kuwa Jina la asili halikuwa na vokali, halijulikani jinsi linavyopaswa kutamkwa. (Kwa mfano, ASV inalitafsiri kama “Yehova,” ambapo tafsiri nyingi za kisasa hulitafsiri kwa urahisi “BWANA” [ili kuitofautisha na Adonai, “Bwana”]). 2. Wanazuoni wa Kiyahudi kwa ujumla hulitamka kama “Adonai” YHWH, kwa kuheshimu utakatifu wake. 3. Linatumika kama jina la kawaida (limetumika mara 6,828 katika Agano la Kale), na wengine wanadhani kwamba linaweza kuhusiana na kitenzi “kuwa” (Rej. Kut. 3:14-15 Bwana anatangaza, “MIMI NIKO AMBAYE NIKO... Bwana ... amenituma kwenu. Hili ndilo jina langu hata milele). 4. Yahweh kama MIMI NIKO anaungana na madai ya “MIMI NIKO” ya Masihi Yesu (rej. Yoh. 6:35; 8:12; 10:9, 11; 11:25; 14:6; 15:1), ambaye alidai kuwa sawa na Yahweh. 5. Yahweh, jina la uhusiano wa kiagano. a. Jina la Agano la Ibrahimu (Mwa. 12:8) b. Jina la Kutoka (Kut. 6:6; 20.2) c. Uhusiano wa kipekee: ingawa majina ya Elohim na Adonai yalijulikana kwa watu wengine, Yehova lilijulikana kimahususi kwa Israeli.

Made with FlippingBook - Share PDF online