Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 1 7 3
M U N G U B A B A
Majina ya Mwenyezi Mungu (muendelezo)
II. Majina Mchanganyiko: Jina la Mungu likihusisha Majina El (au Elohim ) na Yehova A. El Shaddai 1. Linatafsiriwa kama “Mungu Mwenyezi.” 2. Pengine linahusiana na neno mlima, likidokeza uweza au nguvu za Mungu 3. Jina la Mungu kama Mungu ashikaye maagano (Mwa. 17:1; rej. mis. 1-8)
B. El Elyon 1. Linatafsiriwa kama “Mungu Aliye Juu Zaidi” 2. Majina haya yanahusu “Ukuu wa Mamla ya Mungu”
3. Yehova Mungu ni mungu juu ya wote wanaoitwa miungu (rej. Mwa. 14:18-22). Melkizedeki alimtambua kama “Mungu Aliye Juu Zaidi” kwa vile yeye ni mmiliki wa mbingu na nchi (ms. 19).
C. El Olam 1. Linatafsiriwa kama “Mungu wa Milele” 2. Linasisitiza asili ya Mungu ya kutobadilika (Mwa. 21:33; Isa. 40:28)
D. Majina ya mchanganyiko na Yehova 1. Yehova - Adonai, “ Bwana Mwenye enzi yote ,” Mwa. 15:2, 8 2. Yehoa Yireh, “ Mungu mpaji ,” Mwa. 22:14
3. Yehova Elohim, “ Bwana Mungu ,” Mwa. 2:4-25 4. Yehova-Nissi, “ Bwana bendera yetu ,” Kut. 17:15 5. Yehova-Rapha, “ Bwana mponyaji wetu ,” Kut. 15:26 6. Yehova-Rohi, “ Bwana mchungaji wetu ,” Zab. 23:1
Made with FlippingBook - Share PDF online