Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

2 0 0 /

M U N G U B A B A

K I A M B A T I S H O C H A 2 8 Kushika Imani, Sio Dini Jitihada za Kiukombozi za Kuzingatia Muktadha Charles Kraft

Makala haya yamechukuliwa kutoka Mission Frontiers: The Bulletin of the US Center for World Mission, Buku la 27, Na. 5; Septemba-Oktoba 2005; ISSN 0889-9436. Copyright 2005 ya taasisi ya U.S. Center for World Mission. Yametumiwa kwa idhini. Haki Zote Zimehifadhiwa.

Yafuatayo yamenukuliwa kutoka sura ya 5 na 6 ya Appropriate Christianity (William Carey Library Publishers, 2005). Haieleweki sana nje ya Ukristo au hata ndani ya Ukristo kwamba imani yetu inakusudiwa kuwa tofauti na dini hizo katika uhusiano wake na utamaduni wa watu wanaoifuata. Ingawa dini kamaUislamu, Uhindu, naUbudha zinahitaji sehemu kubwa ya utamaduni ambamo zilizaliwa, Ukristo ukieleweka katika usahihi wake, hauko hivyo. Yesu alikuja kuleta uzima (Yn. 10:10), sio dini. Ni watu ambao wameishusha imani yetu kuwa dini na kuisafirisha kana kwamba ni mshindani tu wa dini zingine. Na kwa hiyo, wale wanaopokea ujumbe wetu wana mwelekeo wa kutafsiri Ukristo kana kwamba ni dini nyingine – dini iliyovikwa vazi la utamaduni – badala ya imani ambayo inaweza kuchukuliwa katika muktadha wa utamaduni wowote. Lakini katika uelewa sahihi Ukristo ni kule kujitoa – na kujitoa huku ni katika mantiki na sio muundo. Hivyo basi, kujitoa kwa Yesu Kristo na maana zinazohusiana na kujitoa huko kunaweza kuakisiwa kivitendo katika miundo mbalibali ya kitamaduni. Hii ndiyo maana nzima ya kuzingatia muktadha. Na hii ni sifa muhimu kabisa ya Ukristo ambayo mara nyingi waenezaji wa Imani hii na vile vile wapokeaji wanaolengwa hushindwa kuieleweka. Sehemu nyingine ya sifa (isiyo njema) ya Ukristo ulimwenguni pote ni kwamba ni jambo la kufikirika zaidi kuliko la kivitendo. Kwa wengi, Imani yetu haihusiani sana na masuala ya maisha halisi kama vile namna ya kupata ulinzi dhidi ya roho waovu, jinsi ya kupata na kudumisha afya ya kimwili na jinsi ya kudumisha uhusiano mzuri na familia. Badala yake, Ukristo mara nyingi huonekana kama sababu ya mivunjiko ya familia. Na wakati ambapo suala ni hitaji la nguvu na ulinzi wa kiroho, hata Wakristo wanahitaji kudumisha uhusiano mzuri na mganga wa kienyeji, kuhani wa imani za kishirikina au tabibu wa tiba za asili kwani, licha ya ahadi za kibiblia, wachungaji Wakristo wanaweza tu kupendekeza njia za kawaida za uponyaji na ulinzi. Ukristo ambao ni sahihi kibiblia na kwa utamaduni kusudiwa utakabiliana na dhana hizi potofu, na kukusudia kuzibadilisha.

Dr. Charles H. Kraft ametumika kama mmishenari nchini Nigeria, alifundisha lugha za Kiafrika na isimu katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan na UCLA kwa miaka kumi, na alifundisha Anthropolojia na Mawasiliano ya Kitamaduni katika kitivo cha Mafunzo ya Kitamaduni cha Fuller Seminary kwa miaka 35 iliyopita. Husafiri sana, amekuwa mwanzilishi katika eneo la muktadha, na hutumiwa sana katika huduma ya uponyaji wa ndani. Ni mwandishi na mhariri wa vitabu vingi, ikiwemo Appropriate Christianity (William Carey Library Publishers, 2005).

Made with FlippingBook - Share PDF online