Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 0 1

M U N G U B A B A

Kushika Imani, Sio Dini (muendelezo)

Wafia Mila

Mjadala wowote wa mada hii unahitaji kuzingatia ukweli kwamba hali ambazo wafanya kazi wengi wanaofanya kazi katika mazingira ya tamaduni mchanganyiko wanafanya kazi katika nyakati hizi ambazo uanzilishi wa makanisa mapya ni nadra sana. Kwa hiyo, sisi tunaofundisha uzingatiaji wa muktadha tunashughulika hasa na wale ambao shauku yao kuu itabidi iwe juu ya jinsi ya kuleta mabadiliko katika hali zilizopo badala ya jinsi ya kupanda makanisa yanayofaa kitamaduni. Hivyo, katika hali ya kawaida, wale wanaojifunza kuzingatia muktadha kunahusu nini wanajikuta wakifanya kazi na makanisa ambayo yamejikita zaidi katika kuzingatia mtazamo wa Magharibi wa Ukristo. Hii imekuwa jadi yao na hawako tayari kuibadilisha. Viongozi wa makanisa mengi kama haya huenda hawakuwahi kuuona Ukristo ufaao kitamaduni na pengine hawana uwezo wa kuufikiria. Na kama wanaweza kufikiria mbinu kama hiyo, hakuna uwezekano wa kutaka kuhatarisha kile wanachokifahamu kwa matumaini ya kupata matokeo yanayofaa kwa utamaduni. Kwa wengi, hatari ya kupoteza nafasi zao inaweza kuwa halisi sana kwa vile wenzao, ambao wamejidhatiti kuhifadhi mila “takatifu” wanaweza kuwageuka na kuwaondoa kwenye parokia zao. Kwa sababu hiyo, tunahitaji kujifunza si tu kanuni za kufaa kitamaduni, lakini kanuni za mawasiliano bora. Na hili linahitaji kuambatanishwa na subira na maombi pamoja na utayari wa kutoa aina sahihi ya mapendekezo ikiwa utahitajika kufanya hivyo. Kikwazo kikubwa kwa wengi, hasa wale ambao wamepokea mafundisho ya kitheolojia, ni hofu kwamba wanaweza kufungua mlango kwa aina potovu ya Ukristo. Wanaona aina mchanganyo wa Ukristo na upagani katika Amerika ya Kusini na kukwepa kile kinachoitwa Ukristo lakini si wa kweli. Kwa kuogopa kwamba wakikengeuka kutoka katika UkristowaKimagharibi ambaowameupokea basi wanajiweka katika hatari ya watu kuyafikisha mambo mbali sana, wanarudi kwenye mambo waliyoyazoea na wala hawafanyi chochote kuyabadilisha, bila kujali kiwango cha kutokuelewa maana halisi ya Ukristo kilichopo katika jamii ya wasioamini. Hofu ya Usawazishaji wa Imani ( Syncretism )

Made with FlippingBook - Share PDF online