Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

2 0 6 /

M U N G U B A B A

Kuweka katika Muktadha Miongoni mwa Waislamu, Wahindu, na Wabudha (muendelezo)

Katika miaka ya hivi karibuni tumekuwa na fursa ya kukutana ya Waislamu kadhaa wa C5, na ingawa asili zetu za kidini na aina za ibada ni tofauti kabisa, tumepata kuwa na ushirika wa kusisimua kabisa katika Isa Masihi. Hakuna mashaka katika akili zetu kwamba Waislamu hawa wa C5 ni washiriki wa Ufalme wa Mungu waliozaliwa mara ya pili, walioitwa kuiishi Injili ndani ya mipaka ya kidini ya jamii zao za asili. Kadri tunavyoendelea kuona mipaka ya C4 katika muktadha wetu, na kadri mzigo wetu kwa Waislamu waliopotea unavyozidi kuwa mzito, tumeshawishika kwamba kielelezo cha imani cha C5 kinaweza kweli kuwa na manufaa kwa majirani zetu wa thamani Waislamu na pengine makundi mkubwa ya ulimwengu wa Waislamu. Sisi wenyewe, tukiwa “Waamini wenye asili ya Ukristo” tunadumisha mtindo wa maisha wa C4, lakini tunaamini kwamba Mungu ametuita kusaidia “kuzaa harakati za C5” katika muktadha wetu… Tumehudhuria mazishi mengi ya Waislamu. Tunahuzunika kila tunapomwona rafiki mwingine Mwislamu akizikwa, akiwa anaenda katika umilele bila wokovu katika Kristo. Kama tulivyoona upinzani dhidi ya kubadili dini na pengo kubwa kati ya jumuiya za Kiislamu na za Kikristo, tunahisi kwamba kupigana vita vya kubadilisha dini ni kupigana vita mbaya. Tuna matumaini kidogo katika nyakati zetu kuamini kwamba kunaweza kutokea mabadiliko makubwa ya kutosha ya kitamaduni, kisiasa na kidini katika muktadha wetu kiasi kwamba Waislamu watakuwa tayari kuingia katika Ukristo wazi wazi na kwa kiwango kikubwa. Lakini tuna tumaini kubwa, kubwa kama ahadi za Mungu, kwamba “harakati za ndani” zinaweza kuibuka – kiasi kwamba idadi kubwa inaweza kugundua kwamba wokovu katika Isa Masihi unamngojea kila Mwislamu ambaye ataamini. Tunaweza kuhisi shauku ya Yesu mwenyewe ya kupeleka “chachu” ya Injili kwenye vyumba vya ndani vya jumuiya za Kiislamu, akiwaita wanaume, wanawake na watoto kutembea pamoja naye kama Bwana na Mwokozi, wakibaki kuwa washiriki muhimu wa familia zao na jumuiya zao za Kiislamu.

Masuala ya Kinadharia na Kitheolojia Kuhusu Harakati za C5

... Nia yetu si kuthibitisha kama C5 inaweza kutokea, kwani mifano halisi inaonyesha kuwa inatokea . Badala yake, tunatumai kusaidia kujenga mfumo wa kuelewa jambo hili na kujibu baadhi ya maswali ambayo yamejitokeza kama vile: Kwa mtazamo wa kibiblia, je, mtu anaweza kuokolewa kweli na kuendelea kuwa Muislamu? Je, mfuasi wa Kristo hahitaji kujitambulisha kama Mkristo na kujiunga rasmi na imani ya Kikristo? Je, mfuasi wa Kristo ambaye ni Muislamu anaweza kuendelea

Made with FlippingBook - Share PDF online