Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 2 0 7
M U N G U B A B A
Kuweka katika Muktadha Miongoni mwa Waislamu, Wahindu, na Wabudha (muendelezo)
kudumisha desturi zote za Kiislamu, hasa kusali msikitini kuelekea Makka na kuendelea kurudia ukiri wa imani ya Kiislamu? Sehemu hii itajengwa katika kauli gezi takribani kumi [zimeelezewa katika toleo kamili la makala haya]. • Kauli-gezi ya 1: Kwa Waislamu, utamaduni, siasa na dini ni vitu ambavyo havitengani kirahisi, na kufanya mabadiliko ya dini huhesabiwa kama kujitenga moja kwa moja na jamii. • Kauli-gezi ya 2: Wokovu ni kwa neema pekee kupitia uhusiano/ukiri wa utii kwa Yesu Kristo. Kubadili dini si sharti wala hakikisho la wokovu. • Kauli-gezi ya 3: Lengo la kwanza la Yesu lilikuwa kusimamisha na kuthibitisha Ufalme wa Mungu, si kuanzishwa kwa dini mpya. • Kauli-gezi ya 4: Neno lenyewe “Mkristo” mara nyingi hupotosha – sio wote waitwao Wakristo wako ndani ya Kristo na sio wote walio ndani ya Kristo huitwa Wakristo. • Kauli-gezi ya 5 : Mara nyingi kuna ombwe kati ya kile watu wanachoamini na kile ambacho dini au makundi yao hufundisha. • Kauli-gezi ya 6: Baadhi ya imani na desturi za Kiislamu zinapatana na Neno la Mungu; nyingine hazipatani. • Kauli-gezi ya 7: Wokovu unahusisha mchakato. Mara nyingi hatua kamili ya uhamisho kutoka ufalme wa giza hadi Ufalme wa nuru haijulikani. • Kauli-gezi ya 8: Mfuasi wa Kristo anahitaji kuwekwa huru na Yesu kutoka katika vifungo vya kiroho ili kustawi katika maisha yake pamoja naye. • Kauli-gezi ya 9: Kwa sababu ya ukosefu wa muundo na mpangilio wa kikanisa, harakati za C5 lazima ziwe na utegemezi wa kipekee kwa Roho na Neno kama chanzo kikuu cha maelekezo. • Kauli-gezi ya 10 : Theolojia inayoendana na muktadha husika inaweza tu kuendelezwa ipasavyo kupitia mwingiliano thabiti wa uzoefu halisi wa huduma, uongozi maalum wa Roho na kujifunza Neno la Mungu.
“Kanisa Huibuka Kutokea Ndani” Wanandoa wamishenari wanaofanya kazi huko Asia wanaripoti, “Mwaka 1990 tulitumwa shambani
kama wapanda makanisa. Lakini katika mwaka uliopita tumeona
kwamba wakati Injili inapopandwa kwenye udongo wenye rutuba ndani ya makundi ya kijamii ambayo tayari yameimarika – kama marafiki wa karibu, au kaya yenye vizazi vingi, kanisa linaibuka kutokea ndani. Sio kwamba tunapanda kanisa, lakini tunapanda Injili, na kadri mbegu ya Injili inavyokua, kanisa au makanisa yanaundwa kulingana na taswira ya mitandao iliyopo.”
Kutazama Zaidi ya Ulimwengu wa Kiislamu
. . . Maktaba ya William Carey imechapisha upya kitabu cha kushangaza kiitwacho Churchless Christianity (Hoefer 2001), yaani Ukristo Bila Kanisa . Mwandishi, alipokuwa akifundisha katika seminari moja huko India alianza kusikia hadithi za
Made with FlippingBook - Share PDF online