Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 1 1

M U N G U B A B A

K I A M B A T I S H O C H A 3 0 Watu Waliozaliwa Upya Ufahamu wa Kimsingi juu ya Harakati za Watu Donald McGavran

Makala haya yamechukuliwa kutoka Mission Frontiers: The Bulletin of the US Center for World Mission, Buku la 27, Na. 5; Septemba-Oktoba 2005; ISSN 0889-9436. Copyright 2005 ya taasisi ya U.S. Center for World Mission. Yametumiwa kwa idhini. Haki Zote Zimehifadhiwa.

Ujumbe wa Mhariri: Zifuatazo ni nukuu kutoka kwenye dibaji ya marehemu Donald McGavran’s katika toleo la Kiingereza la kitabu kizuri sana cha Christian Keysser’s, Watu Waliozaliwa Upya (William Carey Library, 1980). Picha ya uandishi wa McGavran na wasifu wa maisha yake unadhihirisha ni kwa kiasi gani watetezi wa leo ama wa harakati za ndani au wale wa harakati za upandaji makanisa wanajenga juu ya misingi iliyowekwa na waanzilishi kama vile Keysser, McGavran na wengine katika nusu ya kwanza ya karne ya 20. Zingatia, katika aya ya mwisho, uchunguzi wa kiutabiri wa McGavran kuhusu umisheni katika karne ya 21. [Christian Keysser] alizaliwa Bavaria mwaka wa 1877, akaenda Kaiser Wilhelm Land (Guinea Mpya ya Mashariki) mwaka wa 1899, na akabaki ndani au karibu na Sattelberg kama mmishenari hadi 1921 aliporudi Ujerumani… Tafsiri halisi ya [Kitabu cha Keysser] ni Kusanyiko Jipya la Guinea. Jina la kweli na bora zaidi ni: Watu Waliozaliwa Upya: Jumuiya Zinazojali, Kuzaliwa na Maendeleo yake… ... Mnamo mwaka 1900 Keysser alijikuta akilihubiria kabila la Kate (linatamkwa Kawtai au Kotte ) katika milima karibu na bahari…. Busara ya Keysser ilitambua kwamba mchakato wa kuwafanya watu kuwaWakristo unapaswa kuhifadhi ufahamu wa watu hawa, na kuugeuza kuwa Ukristo wa Kikabila au Ukristo wa Jadi... Mnamo mwaka 1935, kwa kiasi kikubwa kupitia maandishi na mihadhara ya [Waskom] Pickett, niliamkia kwenye kufuasa vikundi vya kikabila. Niliandamana naye alipokuwa akifanya utafiti kuhusu umisheni huko Mid-India na kuchangia sura kadhaa kwenye uandishi wake wa kitabu cha Umisheni wa Kikristo katika Mid India , 1938. Mimi, pia, niliona kwamba lengo halikuwa uongofu wa mtu mmoja baada ya mwingine kutoka katika matabaka na makabila, bali ni uongofu wa vikundi vya kijamii vilivyobakia kuwa sehemu ya tabaka au kabila, na kuendelea kuishi katika nyumba za mababu zao. Kwa miongo miwili iliyofuata nilifanya kazi katika kuhimiza harakati za watu wa Satnami kukua – na nilishindwa. Mnamo Harakati za Watu kwa Kristo

Made with FlippingBook - Share PDF online