Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

2 1 2 /

M U N G U B A B A

Watu Waliozaliwa Upya (muendelezo)

mwaka wa 1955, kitabu changu cha Bridges of God kiliita mienendo ya kitabaka au ya kikabila kuelekea Imani ya Kikristo “harakati za watu”.... Kile ambacho Keysser, Pickett na [Bruno] Gutmann walikuwa wameeleza huko New Guinea, India na Tanganyika – Bridges of God – kwa mchango mkubwa wa Pickett pekee, kilielezea kwa lugha ya jumla. Ugunduzi wetu sote ulikuwa kwamba maamuzi ya kikundi, ambayo yalihifadhi maisha ya ushirika wa jamii na kuwezesha wanaume na wanawake kuwa Wakristo bila kutengwa na jamii, imekuwa njia ambayo wanadamu wengi wameingia katika Imani ya Kikristo kutokea kwenye imani zisizo za Kikristo, na imekuwa njia nzuri. Kwa sisi sote wanne, ugunduzi huo ulikuwa mgumu kwa sababu wamishenari walitoka katika sehemu zenye imani thabiti zaidi za Kanisa la Magharibi. Walikuwa wamejifunza kwamba Wakristo wa kweli ni wale ambao kibinafsi na kwa gharama kubwa wanamwamini Yesu Kristo, kumpenda, kutii neno lake, na kujitosa peke yao kuvuka bahari saba kutimiza agizo lake. Waliamini kwamba “mmoja-mmoja dhidi-ya-wimbi” ndiyo ilikuwa njia sahihi, bora zaidi, na mara nyingi ndiyo njia pekee ya watu kufanyika Wakristo. Ugunduzi wa Keysser mnamo 1903 unapaswa kutazamwa kama unaokinzana na imani yake ya siku zote isiyo sahihi. Alitengua mtizamo huo na kugundua kwamba kitendo cha makundi ya watu kuja kwa Kristo “huku wakihifadhi muundo wao wa kijamii” kilikuwa njia bora zaidi. Bila shaka, aliendelea kueleza jinsi ambavyo harakati kama hizo za watu zinapaswa kulelewa, kulindwa dhidi ya urasmi, kulishwa Neno, na kuimarishwa kwa kutumia mara kwa mara chaguzi zake za Kikristo. Huu ni mchango wake mkubwa. Kitabu chake ni muhimu kusoma kwa yeyote anayetaka kuelewa a) kwamba kufuasa makundi ya kikabila ni njia nzuri sana ya kuwafanya watu wengi kuwa Wakristo, na b) namna ambayo kufuasa na kuwakamilisha wengine kunaweza kufanyika ili matokeo yawe ni Wakristo wa kweli katika Kutaniko la Kikristo la kweli – Ushirikia wa Kanisa la kweli lenye muundo mmoja.

Mfikiriaji Huru

. . . Harakati za watu kuhamia katika Ukristo kweli zilianza kuongezeka. Koo na vijiji vya mbali viliingia kwa fujo katika Ukristo, kwa sababu tu waliona kwamba Wakristo walikuwa wamebadilika sana na kuwa bora . Hii ndiyo sababu ya msingi kwa nini harakati za watu hutokea. Wanadamu wanaakili nyingi sana. Hata hivyo mtu ni kiumbe mwenye busara. Anapoona kwamba utaratibu mpya, Kanisa, kiuhalisia

Made with FlippingBook - Share PDF online