Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 7 1

M U N G U B A B A

Prolegomena Fundisho kuhusu Mungu na Kuenea kwa Ufalme

MAELEZO YA MKUFUNZI 1

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa Somo la 1, Prolegomena: Fundisho kuhusu Mungu na Kuenea kwa Ufalme. Lengo la jumla la moduli ya Mungu Baba ni kuwasaidia wanafunzi wako kufahamu mawazo muhimu yanayohusiana na Fundisho kuhusu Mungu, na hasa Fundisho kuhusu Mungu Baba Mwenyezi. Kusudi la somo hili si la kitaaluma kwanza, bali ni kuwatia moyo wanafunzi wako kumtafuta Bwana katika misingi ya Kweli ya Maandiko. Tafadhali, katika somo hili jaribu kutofautisha kati ya ujuzi kuhusu Mungu, na ujuzi wa Bwana kwa imani katika Yesu Kristo. Elimu ya kitaaluma juu ya Bwana ina nafasi yake, lakini haipaswi kamwe kuengua au kufunika ukweli kwamba ujuzi wa Maandiko ni kwa ajili ya kuimarisha maisha ya mtu amtafutaye Bwana ili aweze kutembea na Mungu, na kisha, kwa njia hiyo, kuwa chombo kiteule ambacho Bwana anaweza kukitumia kutenda kazi yake. Ni Baraka ya ajabu namna gani kushiriki katika kujifunza kiakili kuhusu Bwana na nafsi yake! Onyo hili halimaanishi kwamba hatupaswi kumpenda Bwana kwa akili zetu zote (rej. Kum. 6:4-6), bali tu ni kwa ajili ya kuonya kwamba ujuzi huleta majivuno bali upendo hujenga (1 Kor. 8:1). Bwana akubariki unapowaongoza wanafunzi hawa katika safari hii ya kusisimua ya kutafakari utukufu usio na kikomo wa Bwana wetu, Mungu Mwenyezi! Tafadhali zingatia kwa makini “Malengo ya Somo” katika kila somo. Kwa namna fulani, hii ndiyo sehemu muhimu zaidi ya muda wako wa ufundishaji katika darasa. Malengo hutengeneza na kutoa maana kwa shughuli zote mbalimbali, na kujenga umakini wakati wote wa kushirikishana, kujifunza, majadiliano, na hata nyakati za maombi. Natumai utapata kuona kwamba malengo yamesemwa wazi na yanaweza kufikiwa. Malengo haya lazima yaongoze kila ambacho wewe kama mshauri unafanya wakati wa kipindi darasani. Hakikisha kwamba unasisitiza malengo ya somo hili katika kila awamu ya majadiliano na uwasilishaji wako, na uwasaidie wanafunzi wako kuyakumbuka wakati wa maswali, mazungumzo, mijadala, na muda wote uwapo pamoja nao. Kadri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo uwezekano wao wa kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya unavyokuwa mkubwa zaidi.

 1 Page 15 Utangulizi wa Somo

 2 Page 15 Malengo ya Somo

Kwa mara nyingine tena, sehemu hii inatoa muhtasari wa malengo ya sehemu zote mbili, inawakilisha muhtasari wa dhana muhimu za somo, na inatoa muhtasari wa

 3 Page 15 Malengo ya Somo

Made with FlippingBook - Share PDF online