Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

2 7 2 /

M U N G U B A B A

tasnifu ya somo hatua kwa hatua. Katika kila kitu unachofanya, jaribu kutafuta namna za kufanya malengo haya yawe hai kwa wanafunzi na kupima ufanisi wao kupitia uwezo wako wa kuyasisitiza kuanzia mwanzo hadi mwisho wa kipindi chako cha darasani. Sisitiza mawazo haya kwa nguvu kwa sababu, katika maana halisi, dhana hizi ndio msingi wa vipindi vyako vya kujifunza katika somo hili. Kila kitu unachojadili, kupendekeza, na kufanya kinapaswa, kwa namna fulani, kurejelea malengo haya. Tafuta namna ya kuyaangazia haya kila mara, ili kuyawekea mkazo kadri unavyoendelea. Ibada hii inathibitisha kwa mara nyingine ushuhuda wa Biblia kwamba kuwepo kwa mbingu na nchi ni ushuhuda wa kuwepo kwa Mungu Baba Mwenyezi. Uumbaji pia hutumika kama taarifa kwa wale wanaojifanya kuwa hakuna ushahidi wa uhalisia wa Mungu katika ulimwengu. Wazo la Mungu kukataa kubishana na watu kuhusu uwepo wake limesisitizwa vya kutosha katika moduli hii yote. Hatujifunzi maarifa ya Mungu ili kumweka kwenye benchi la mahakama aweze kujibumashtaka, bali ili tukubali kwamba tunamhitaji Yeye aliyeMuumba na Bwana wetu pia. Wazo kwamba Mungu anatakiwa kujitetea mbele na dhidi ya uumbaji wake ni wazo ambalo Biblia inaliita la kipuuzi. Hivyo, ibada tangu mwanzo wake, inatafuta kuweka wazi kwamba katika kujifunza kuhusu Mungu, Bwana kamwe hasimamishwi mahakamani. Kama Bwana na Muumba, vitu vyote ni vyake, nasi ni mali yake. Unyenyekevu lazima utawale kila awamu ya kile tunachofanya katika somo letu kuhusu Bwana. Zab. 24:1-2 – Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. 2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. Kum. 10:14 – Tazama, mbingu ni mali za Bwana, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo. 1 Nya. 29:11 – Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote. Ayu. 41:11 – Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.

 4 Page 15 Ibada

Made with FlippingBook - Share PDF online