Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 7 5

M U N G U B A B A

mwangalifu hasa ikiwa wanafunzi wako watavutiwa na mawazo fulani na watataka kuendelea na mjadala kuhusu mambo ambayo ni ya kimungu lakini hayahusiani na somo. Ruhusu muda unaofaa wa kuangazia mambo muhimu, na bado uwe na muda wa kutosha wa mapumziko kabla ya sehemu inayofuata ya video kuanza.

Kuwasaidia wanafunzi wako kuelewa mipaka ya akili katika kumtafuta Mungu ni mojawapo ya kazi muhimu zaidi kwa mkufunzi wakati wa kujifunza moduli hii. Katika hili tunaweza kujifunza kutoka kwa wanatheolojia wakuu wa historia. Zifuatazo ni nukuu mbili kutoka kwa Anselm, askofu wa kale wa kanisa katika karne ya 11, ambaye maoni yake kuhusu upitaji mipaka wa Mungu yalimsaidia kuweka malengo ya kweli katika kujifunza kwake kuhusu Mungu Baba Mwenyezi. Nukuu hizi zote mbili zinasisitiza haja ya mwanafunzi wa Neno la Mungu kuwa mnyenyekevu; si kutafuta kuelewa ili kuamini, bali kuamini ili kuelewa . Sijaribu, Bwana, kupenya katika utukufu wako, kwa maana ufahamu wangu haufikii hilo. Lakini ninatamani kwa kiasi fulani kuelewa kweli yako, ambayo moyo wangu unaamini na kuipenda. Kwa maana sitaki kufahamu ili nipate kuamini, bali naamini ili nipate kuelewa. Kwa maana hili nalo naamini, ya kwamba nisipoamini, sitaelewa. ~ Anselm. Proslogion 1 Mpangilio sahihi ni kuamini mambo mazito ya imani ya Kikristo kabla ya kuanza kuyajadili kwa ufahamu wa kawaida. Lakini tunaghafilika ikiwa, tukiwa tumeufikia uthabiti wa imani, hatutafuti kuelewa kile tunachoamini. Kwa neema ya Mungu iliyotangulia na kuniandaa kwa ajili ya wokovu, ninajiona kushikilia imani ya ukombozi wetu, ili hata kama ningeshindwa kabisa kuuelewa, kusiwe na kitu kinachoweza kutikisa uthabiti wa imani yangu. Tafadhali nionyeshe ni nini, kama unavyojua, wengine wengi wote pia wanatafuta kujua: Kwa nini Mungu, ambaye ni muweza wa yote, achukue udogo na udhaifu wa asili ya mwanadamu ili kuifanya upya? ~ Anselm. Cur Deus Homo (Boso to Anselm) 1:2

 9 Page 26

Muhtasari wa Sehemu ya 2

Made with FlippingBook - Share PDF online