Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
2 7 6 /
M U N G U B A B A
Sehemu hii ni muhimu kwa ajili ya kutoa muhtasari wa dhana zote muhimu zilizotolewa katika sehemu za ufundishaji wa video. Kweli hizi zinawakilisha kweli za msingi ambazo wanafunzi wanapaswa kuwa wamezifahamu kupitia mijadala, kujifunza, kusoma vitabu vyao vya kiada na kupata kutoka katika vyanzo vingine vya somo hili. Ikiwa unataka kufanyia mazoezi haraka mawazo muhimu ya somo pamoja na wanafunzi, hii ndiyo sehemu ambayo unapaswa kupitia. Orodha hii basi inakuwa marejeleo rahisi yaliyo tayari ya mawazo makuu kwa kila somo. Hakikisha kuwa dhana hizi zimefafanuliwa kwa uwazi na kuzingatiwa kwa uangalifu, kwa sababu kazi yao ya jaribio na mitihani itachukuliwa moja kwa moja kutokana maarifa haya. Mojawapo ya tabia muhimu zaidi za kukuza kwa wanafunzi wako ni uwezo sio tu wa kujua maudhui yaliyomo katika nyenzo mbalimbali, lakini kugundua muktadha mpya ambamo kweli zinazopatikana katika maudhui hayo zinaweza kutumika na kuhamishiwa. Matumizi yenye ubunifu wa kweli yanadai utayari wa kubaini maeneo ya uhusianishaji, kufanya matumizi pendekezwa, kufikiria kupitia hali na mazingira yao wenyewe ili waweze kushughulika na kujihusisha na maarifa husika kwa kiwango kipya cha umakini na uzingativu. Kanuni ya msingi kwa sehemu hii ni rahisi: maswali bora zaidi ni yale ambayo ni muhimu kwa wanafunzi mahali walipo . Kilicho muhimu hapa sio maswali yaliyoandikwa hapa chini, bali ni wewe kushirikiana na wanafunzi kutatua masuala, mashaka, maswali na mawazo ambayo yanatokana moja kwa moja na uzoefu wao, maisha na huduma zao. Usisite kutumia muda wa kutosha kwa ajili ya swali fulani linalotokana na video, au masuala fulani maalum ambayo yanaendana na muktadha wa huduma zao za hivi sasa. Lengo la sehemu hii ni wewe kuwasaidia kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na mazingira ya huduma zao. Kwa mara nyingine tena, maswali yaliyo hapa chini yametolewa kama miongozo na vitangulizi, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Chukua na chagua kati ya hayo, au uje na ya kwako mwenyewe. Jambo muhimu ni yawe yanayofaa sasa kwa muktadha na maswali yao.
10 Page 35 Muhtasari wa Dhana Muhimu
11 Page 36 Kutendea Kazi Somo na Matokeo Yake kwa Mwanafunzi
Made with FlippingBook - Share PDF online