Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 7 7

M U N G U B A B A

Uchaguzi huu wa mifano umetokana na uzoefu katika hali halisi za huduma, na unaonyesha aina za matumizi ya mafunzo ambayo wanafunzi wako wanaweza kukutana nayo wanapohudumu. Jambo muhimu kuhusu mifano hii ni kwamba haijawekwa kwenye uelekeo wa kitaaluma . Ingawa inahusisha maswali na masuala kadhaa yanayohusiana na jinsi watu wanavyoona na kuelewa hali za maisha yao, kiini hasa cha mifano hii ni hekima katika kutumia Kweli ya Injili kwa hali fulani katika muktadha maalum. Kazi yako kama mkufunzi katika mifano halisi ni kuwasaidia wanafunzi kuchunguza njia ambazo kweli wanazojifunza zinaweza kuchukuliwa na kutumiwa katika hali fulani . Waruhusu watengeneze matukio, na kufikiria matokeo ya masuluhisho tofauti wanayoweza kupendekeza. Lengo hapa ni kuwasaidia wanafunzi kuanza kufikiri kama viongozi wanavyofikiri. Mara nyingi zaidi matumizi ya Neno huhitaji uwazi kwa Bwana na ufahamu wa hali husika ili Roho aweze kukuwezesha kutumia Kweli ipasavyo. Kazi yako kama mshauri si lazima kuwa mtaalamu wa kila swali ambalo wanafunzi wanalo, bali ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaendelea kusoma nyenzo na kufanya kazi. Hakikisha unajua mapema kile kinachohitajika kutoka kwa wanafunzi juma lijalo, na uwe na taarifa stahiki na nyenzo ambazo watahitaji ili kukamilisha kazi zao za juma lijalo. Hii ni kazi muhimu sana kwa uzoefu wao wa kujifunza, na, tunashukuru, sio ngumu kufanya. Kuhusiana na kazi zao za kusoma, wakumbushe wanafunzi wako kwamba lengo ni kwamba wasome nyenzo kadri wawezavyo, na kisha waandike sentensi chache juu ya kile wanachoamini kuwa mwandishi alikuwa anajaribu kuwasilisha. Ingawa kujifunza moduli hii hakutegemei sana usomaji huu unaoagizwa, bado ni ujuzi muhimu wa kiakili kwa wanafunzi wako kujifunza kuchakata mawazo ya wengine. Kwa hiyo, tumia wakati vizuri kuhimiza juhudi zao katikamchakato huu. Bila shaka, kwa wale wanafunzi ambao wanaweza kupata ugumu au kutoweza kumaliza kazi, wahakikishie dhamira ya zoezi hili , na usisitize ushiriki wao darasani kama ufunguo wa kujifunza kwao, si ujuzi wao wa kusoma au kuandika. Tunapoomba kwa ajili ya wanafunzi tutafanya pia bidii ya kumsaidia kila mwanafunzi kuboresha stadi hizo, tunataka kukazia kujishughulisha kwa wanafunzi katika Maandiko kuwa ndicho kiini cha kozi hii. Hata katika mwanga wa hili, tusidharau uwezo wa wanafunzi wetu. Hapa, jitaidi kutafuta uwiano kati ya kuwapa changamoto na kuwatia moyo.

 12 Page 37 Uchunguzi Kifani (Mifano Halisi)

 13 Page 40 Kazi

Made with FlippingBook - Share PDF online