Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 7 9

M U N G U B A B A

Mungu kama Muumba Utawala wa Mungu

MAELEZO YA MKUFUNZI 2

Karibu katikaMwongozowaMkufunzi kwa ajili ya Somo la 2, Mungu kamaMuumba: Utawala wa Mungu. Katika somo hili muhimu lengo lako litakuwa kuwasaidia wanafunzi wako waelewe baadhi ya njia ambazo Mungu Baba Mwenyezi hutumia mamlaka yake kuu ya utawala juu ya uumbaji wake. Maandiko mengi ya Biblia yanazungumza juu ya uangalizi, ulinzi, uhifadhi, na utawala wa Mungu juu ya ulimwengu kwa nguvu na hekima yake. Maandiko machache tu yanatosha kuamsha shauku zetu kuhusu uangalizi na utunzaji wa ajabu wa Mungu wetu mkuu juu ya uumbaji wake. Zab. 135:5-7 – Maana najua mimi ya kuwa Bwana ni mkuu, Na Bwana wetu yu juu ya miungu yote. 6 Bwana amefanya kila lililompendeza, Katika mbingu na katika nchi, Katika bahari na katika vilindi vyote. 7 Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika hazina zake. 1 Nya. 16:31 – Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, “Bwana ametamalaki!” Zab. 33:14-15 - . . . toka mahali pake aketipo Huwaangalia wote wakaao duniani. 15 Yeye aiumbaye mioyo yao wote Huzifikiri kazi zao zote. Zab. 47:7 – Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili Unapowaongoza wanafunzi kupitia kweli hizi na nyingine zinazohusiana na hizi, hakikisha kwamba kweli hizi zinawaongoza kumstaajabia Mungu, kumwabudu, kutambua katika maisha yao kwamba Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu ni Mungu anayestahili sifa na heshima. Somo hili hasa ni muhimu kwa wale wanaomtumikia Bwana katikati ya hali na mazingira magumu, ambao wanaishi katika nyakati ambazo zinaonekana kana kwamba uovu unashinda, nguvu za Mungu hazipo na nguvu za uovu ni kubwa na zina uwezo wa kuleta uharibifu mkubwa. Unaposisitiza malengo yako katika somo hili, jaribu kuweka hesabu ya kiakili ya jinsi unavyoweza kuongoza mjadala ili kuwawezesha wanafunzi wako kutumia kweli zinazohusu utunzaji na uhifadhi wa Mungu katika nyakati na vipindi vya mateso na hasara. Hili lina matumizi maalum kwetu katika huduma za maeneo ya mijini.

 1 Page 45 Utangulizi wa Somo

Made with FlippingBook - Share PDF online