Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

2 8 0 /

M U N G U B A B A

W. B. Pope anasisitiza umuhimu wa utunzaji na uhifadhi wa Mungu katika elimu ya dini anaposema: Uhifadhi ni neno pana zaidi katika lugha ya kitheolojia. Ni usuli wa idara zote kadhaa za ukweli wa kidini, usuli ambao ni fumbo katika mchanganyiko wake wa mng’aro na giza. Unapenya na kujaza dira nzima ya mahusiano ya mwanadamu na Muumba wake. Unaunganisha Mungu asiyeonekana na umbaji unaoonekana, na uumbaji unaoonekna na kazi ya ukombozii, na ukombozi na wokovu binafsi, na wokovu binafsi na mwisho wa mambo yote. Huyarudisha mawazo yetu hadi kwenye kusudi kuu lililokuwa hapo mwanzo na Mungu, na kuyapeleka mbele hadi mwisho unaotazamiwa na utimilifu wa mambo yote, huku ukijumuisha kati ya haya aina mbalimbali zisizo na kikomo za shughuli za Mungu na mwanadamu. ~ W. B. Pope. Compendium of Christian Theology, I. uk. 456 . Somo lenye kina kama hili linahitaji bidii na unyenyekevu wote. Ibada hii inakazia ukuu wa Mungu wetu katika utawala wake usio na mipaka na umiliki wa vitu vyote. Uangalizi na utunzaji waMungu juu ya ulimwengu unahusisha viumbe na vitu vyote, unahusisha kiroboto mdogo zaidi hadi nyangumi mkubwa zaidi, na kugusa sharubu kwenye nyuso zetu hadi kwenye galaksi iliyo mbali zaidi kwa matrilioni na matrilioni ya matrilioni ya maili. Utunzaji wa Mungu ni kama asili yake – hauna mwisho na ni wa kushangaza. Zaburi 145 inatoa taarifa na muhtasari mzuri wa uhifadhi na utunzajii wa ajabu wa Mungu juu ya vitu vyote katika ulimwengu: Zab. 145:9-13 – Bwana ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. 10 Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi. 11 Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako. 12 Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. 13 Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. [Bwana ni mwaminifu katika maneno yake yote, na mwenye fadhili katika kazi zake zote.]

 2 Page 46 Ibada

Made with FlippingBook - Share PDF online