Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 2 8 1
M U N G U B A B A
Hakuwezi kuwa na Mungu mwingine ila Mungu mmoja tu, Muumba mmoja wa miisho ya dunia wa kweli na Aliye Hai. Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, YHWH, Baba Mwenyezi ndiye Bwana huyu wa kweli. Umoja, wa pekee, na mkuu, na sasa, Mungu wetu kwa imani katika Yesu Kristo.
Katika kupitia upya maswali na wanafunzi kila mara zingatia dhana kuu ambazo maswali yanalenga kuibua. Jihadhari na tabia ya wanafunzi kutaka kukariri maswali, kubishana kwa hoja zao, au kutilia shaka uhalali wa swali lenyewe. Kilicho muhimu kujua ni kwamba maswali ni chombo cha kufanya marudio. Suala la msingi ni kweli wanazotakiwa kujifunza, na ikiwa watafanikiwa kuzijua kweli hakika watajua majibu. Ingawa hii inaweza kuonekana kuwa rahisi, ni wazo ambalo mara nyingi wanafunzi hawalizingatii. Mifano ya rejea katika eneo hili inalenga wazo la uwepo wa Mungu na udhibiti wake juu ya hali na masuala ambayo hutoka nje ya uwezo wa mwanadamu. Kama lipo jambo lisilobadilika kuhusu hali ya maisha na huduma kwenye maeneo ya mjini ni kwamba hakuna kitu kama kutobadilika. Watu wengi wa mijini wanaishi katika hali ambazo zinawaweka hatarini kila wakati, wakipitia mambo yasiyo ya haki na mara nyingi ya kutisha, bila dalili kwamba kuna mtu anayejali au hata anayejua maumivu yao. Kujifunza somo la uhifadhi na utunzaji wa Mungu miongoni mwa watu wa mjini ni kuuliza swali la sababu ya uwepo wa uovu ( theodicy ) , wazo la kwa nini mambo mabaya huwapata watu wema. Angazia pamoja na wanafunzi wako mawazo ya uhifadhi na utunzaji wa Mungu kama mwongozo katika kuchunguza baadhi ya ushahidi wa kibiblia kuhusu somo hilo. Nia yako katika sehemu hii ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa muhtasari wa jumla wa fundisho la Maandiko kuhusu uhifadhi na utunzaji wa Mungu kama ulivyowasilishwa katika sehemu ya kwanza ya video. Kwa namna fulani ugumu wa kuelewa utunzaji mkuu wa Baba ni jambo la kawaida kwetu; akili yoyote inawezaje kuelewa kusudi kuu la Mungu la kuleta uumbaji wote chini ya utawala wake ili kutimiza kusudi lake kuu la uumbaji, ambalo si lingine zaidi ya kuanzishwa kwa utawala wa ufalme wake katika ulimwengu wote mzima (Efe 1:9-11; Kol. 1:19-20).
3 Page 47 Jaribio
4 Page 48 Mifano ya rejea
5 Page 55 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook - Share PDF online