Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
2 8 2 /
M U N G U B A B A
Wasaidie wanafunzi kupitia upya mafundisho ya video ili waweze kuwa na ubobevu wa dhana za msingi zilizozungumziwa ndani yake. Zingatia kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa majibu kulingana na malengo ya somo la sehemu ya kwanza. Aina hii ya mapitio ni muhimu kwao kwa ajili ya kujenga uelewa wao wa kweli hizi wanapoendelea. Kama kawaida, kuwa mwangalifu katika matumizi yako ya muda, ukizingatia mawazo muhimu na kuangalia barabara zote za pembezoni au mitaro ambayo inaweza kukufanya usifanyie mazoezi kweli muhimu na mambo makuu ya utunzaji wa Mungu. Katika kupitia pamoja na wanafunzi kweli za sehemu hii, hakikisha unapitia pamoja nao kwa haraka baadhi ya nadharia mbadala zinazozunguka kuwepo kwa Mungu wa utunzaji wake duniani. Mtazamo wa kiatheisti (au materialistic) unashikilia dhana kwamba hakuna Mungu, na kwamba ulimwengu unaoonekana ni wa milele. Huu ni mtazamo maarufu wa kimageuzi usioamini kuhusu Mungu, ambao unadai kwamba ulimwengu unaoonekana ulijikusanyia wenyewe kila kitu kilichohitajika kuifanya mbingu na nchi vitokee kupitia mchakato wa mageuzi wa muda mrefu. Mtazamo wa kipantheisti husema Mungu ni kila kitu na kila kitu ni Mungu. Dhana hii inashikilia kwamba ulimwengu ni kama “vazi hai” la Mungu, ambaye ni nafsi ya ulimwengu, ambao ni uummbaji na muonekano wa kimwili wa umbo lake. Katika mtazamo huu Mungu anafanywa kuwa sawa na ulimwengu wenyewe, na unatofautiana kidogo na maoni ya kimaterialisti . Mtazamo wa uungu unashikilia kwamba Mungu yuko, aliumba vitu vyote, lakini kwamba, aliviumba kwa namna ambayo havihitaji ushiriki wala uangalizi wake katika kuendelea kwake. Mungu aliufanya ulimwengu wa kimwili kuwa chini ya sheria au kanuni fulani zisizobadilika ambazo huzitii, lakini wanadamu hudumisha uhuruwao kamawakala huru “wenye ufahamunamaadili.”Mfanowamtengenezaji wa saa hutumiwa mara nyingi kuelezea mtazamo huu: Namna Mungu alivyo kwa uumbaji wake ni kama mtengenezaji wa saa anavyofanya kwenye saa yake. Mungu alitengeneza saa, akamaliza, na kuiacha peke yake. Mungu ni mkuu asiyejihusisha na mambo ya wanadamu; dini ya kweli kwa mtazamo huu, ni dini ya asili tu. Sheria
6 Page 65 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook - Share PDF online