Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 8 3

M U N G U B A B A

na taratibu au michakato ya asili ndiyo namna ya juu kabisa tunayoweza kwenda katika kuielewa nafsi na nguvu za huyu Mungu asiyekuwepo ulimwenguni. Unapochunguza maana za sehemu ya pili, hakikisha kwamba unawasaidia wanafunzi kung’ang’ania njia ambayo ufahamu wa kibliblia wa utunzaji wa Mungu unatoa uelewa wa jinsi tunavyoweza kuzikabili na kuzipinga njia nyingine mbadala wa tamko rahisi la Biblia kwamba Baba Mwenyezi anasimamia ulimwengu wake. Mifano yote hii halisi inatafuta kufukua baadhi ya mapingamizi dhidi ya fundisho la kibiblia la utunzaji na uhifadhi wa Mungu. Katika wakati huu wa vurugu kubwa, sayansi yenye usumbufu, na udhalilishaji wa kijinsia, ni ngumu mara nyingine kusisitiza kwamba “Mungu wetu anatawala.” Matokeo ya asili ya kulisisitiza hili mbele ya ukorofi na ukatili wa kutisha namna hii ni kuuliza Mungu anatawalaje hasa . Kujadili mawazo haya ni muhimu, kwani bila kuwa na angalau muktadha wa kuyajadili, hapawezi kuwa na njia yoyote ya kujibu hoja za upinzani. Wanafunzi leo hii ni lazima wajifunze kutii 1 Petro 3:15: “na mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu.” Kwamara nyingine tena, lengo kwa ajili ya wanafunzi wako ni uwezowa kukabiliana na kweli ya Mungu na kuweka wazi jinsi mapingamizi na makanusho ya wale wanaokataa mtazamo wa kibiblia yanaweza kujibiwa. Shauku hapa si kubishana na adui zetu bali ni kuifanya kweli iwe wazi sana kiasi kwamba hata mkaidi ni lazima angalau akiri uhalali wa ukweli wa Maandiko. Kusema ukweli, uongofu ni wajibu wa Mungu, kueleza ukweli ili wengine waweze kuelewa waziwazi ni wajibu wetu. Zab. 119:46 – Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu. Kol. 4:6 – Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu. 2 Tim. 2:25 – ... akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli.

 7 Page 68 Uchunguzi Kifani

Made with FlippingBook - Share PDF online