Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
2 8 4 /
M U N G U B A B A
Katikati ya kiini kabisa cha somo hili pana uhitaji wa kukabiliana na utofauti kati ya yale ambayo Maandiko yanazungumza kuhusu watu wa Mungu na yale yanayoonekana kuwa yanatendeka katika maisha yao . Suala hili, pambano hili, huibua wingi wa mijadala na shughuli za wale wanaohubiri Habari Njema kwa wakazi wa mijini, ambao wengi wao maisha yao ni mzigo na uchungu daima. Je, watumishi wa mijini watawaambia nini wale ambao maisha yao yanaonekana kuharibiwa na kuumizwa, yakikabiliwa na hatari ya maumivu ya kila aina na uharibifu usiofikirika? Kama wahudumu wa neema ya Mungu katika Kristo, ni lazima wajifunze kuelewa vema utunzaji na uhifadhi wa Mungu ili waweze kuushuhudia upendo wa Mungu, na bado, pia waweze kuzungumzia kuwepo kwa ulimwengu, mwili, Ibilisi, na uwezo wao wa kuingilia na kupingana na mapenzi ya Mungu. Mapambano haya ndicho kiini cha theolojia yoyote halali ya mijini, kuweka wazi jinsi utunzaji na upaji mwema wa Mungu unavyoweza kujibu changamoto na mahitaji yanayowakabili wale wanaoishi katika miji hatari ya ulimwengu. Weka jukumu hili kuu katika akili yako unapotafuta kuwaongoza wanafunzi katika mazungumzo ya wazi kuhusu Neno la Mungu. Omba kwa ajili ya wanafunzi wako kila mara upatapo nafasi, katikati ya juma au wakati wa kipindi cha darasa. Kamwe usichukulie maombi kikawaida; kwa kila namna, maombi yanaweza kuleta matokeo makubwa katika maisha ya wanafunzi wako. Neno la Mungu liko wazi kwamba Roho Mtakatifu anaweza kuwafundisha na kuwaongoza katika kweli: 1 Yoh. 2:20 – Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote 1 Yoh. 2:27 – Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake. 1 Yoh. 4:13 – Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. 1 Kor. 2:13 – Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima
8 Page 69 Marudio ya Tasnifu ya Somo
9 Page 70 Ushauri na Maombi
Made with FlippingBook - Share PDF online