Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 8 5

M U N G U B A B A

ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. 1 Thes. 2:13 – Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini. Tarajia Roho Mtakatifu kuwaongoza wanafunzi katika kweli yote wanapojadili na kuchunguza Neno la Mungu pamoja. Kamwe usichukulie kuwa ni jambo la kawaida sana au lisilo la lazima kuwauliza wanafunzi kama wanahitaji maombi kwa ajili ya mtu fulani au jambo linalohusiana na mawazo na kweli ambazo zinapatikana katika somo. Maombi ni njia ya ajabu ya vitendo na yenye msaada ya kutumia kweli; kwa kuyapeleka mahitaji fulani maalum mbele za Mungu katika mwangaza wa kweli, wanafunzi wanaweza kuimarisha mawazo hayo katika nafsi zao, na kupokea tena kutoka kwa Bwana majibu wanayohitaji ili kutegemezwa katikati ya huduma zao. Bila shaka, kila kitu kwa kiasi fulani kinategemea kiasi cha muda ulionao katika kipindi, na namna ulivyoupanga. Bado, maombi ni sehemu muhimu na yenye nguvu ya kila mguso na mafudisho ya kiroho, na kama unaweza, yanapaswa kuwa na nafasi yake kila wakati, hata kama ni maombi mafupi ya muhtasari wa yale ambayo Mungu ametufundisha, na azimio la kuishi kulingana na kweli zake kama Roho Mtakatifu anavyotuongoza.

Made with FlippingBook - Share PDF online