Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 8 9

M U N G U B A B A

Ushuhuda wa Daudi katika Zaburi ndogo ya 131 ni mgodi wa kweli wa dhahabu wa ufahamu kwa ajili yetu tunapotafuta kuzama ndani ya kina cha nafsi ya Bwana mwenyewe: Zab. 131:1-3 –Bwana, moyowangu hauna kiburi,Walamacho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu. 2 Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa Kifuani mwa mama yake; Kama mtoto aliyeachishwa, Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu. 3 Ee Israeli, umtarajie Bwana, Tangu leo na hata milele. Hebu basi tusisitize lugha ya Biblia iliyowazi kabisa: Mungu ni mmoja. Kum. 6:4 – Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja 1 Fal. 8:60 – . . . Watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa Bwana ndiye Mungu; hakuna mwingine Isa. 44:6 – Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. Lakini acha pia tuweke msisitizo kwamba Yesu ni Neno aliyefanyika mwili (Yoh. 1:14), na tumthibitishe Roho Mtakatifu kama Bwana na mpaji wa uzima kwa Kanisa (2 Kor. 3:17-18). Tuwape nafasi waandishi wa vitabu vyetu kuwa na neno la mwisho hapa: Kanisa halijasita kufundisha fundisho la Utatu. Bila kujifanya kwamba linaelewa, limetoa ushahidi wake, limerudia yale ambayo Maandiko Matakatifu yanafundisha. Baadhi wanapinga wakisema kwamba Maandiko hayafundishi Utatu wa Mungu kwa msingi kwamba wazo zima la Utatu katika umoja ni mkanganyiko wa maneno; lakini ikiwa hatuwezi kuelewa kuanguka kwa jani kando ya barabara au kuanguliwa kwa yai la ndege kwenye kiota kule, kwa nini Utatu uwe tatizo kwetu? “Tunamfikiria Mungu kwa kiwango cha juu zaidi” anasema Michael de Molinos, “kwa kujua kwamba yeye hawezi kueleweka, na yuko juu ya ufahamu wetu, kuliko kumwelewa katika picha yoyote, au uzuri wa kiumbe chochote, kulingana na fahamu zetu potofu.”

~ A.W. Tozer. The Knowledge of the Holy. New York: Harper San Francisco, 1961. uk. 18-19.

Made with FlippingBook - Share PDF online