Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

2 9 0 /

M U N G U B A B A

Kanisa linaimba, “Utukufu kwa Baba, na kwa Mwana, na kwa Roho Mtakatifu.” Hii ni nini? Tunaomba na kutoa sifa kwa miungu watatu? Hapana; sifa kwa Mungu mmoja katika nafsi tatu. Kama vile wimbo unavyosema, “Yehova! Baba, Roho, Mwana! Uungu wa Ajabu! Utatu katika Umoja!” Huyu ndiye Mungu ambaye Wakristo humwabudu – Yehova wa Utatu. Kiini cha Imani ya Kikristo kwa Mungu ni ajabu iliyofunuliwa ya Utatu. Trinitas ni neno la Kilatini lenye maana ya utatu. Ukristo unasimama juu ya msingi wa fundisho la trinitas, sifa ya utatu, nafsi tatu za Mungu.” ~ J. I. Packer. Knowing God. Downers Grove: InterVarsity Press, 1993. uk. 65. Katika wakati ambao fundisho rasmi la ufunuo wa Mungu linachukuliwa kama “mzigo wa kitheolojia” ni muhimu kuwakumbusha wanafunzi juu ya kile kilicho hatarini kwa habari ya imani sahihi juu ya Mungu. Vitabu hivi vya marejeleo vyote viwili vinathibitisha umuhimu wa kumwona na kumwelewa Mungu sawasawa, kwa kupatana na kile ambacho amejidhihirisha kuwa kwetu. Wajibu wetu ni kugundua jinsi Mungu alivyo, na si vile tunavyomfikiria kuwa, na tunavyomtaka awe. Kwamba fikra zetu kuhusu Mungu zinalingana karibu iwezekanavyo na hali halisi ya Mungu ni jambo la umuhimu mkubwa sana kwetu. Kauli zetu za ukiri wa imani hazina umuhimu mkubwa wala matokeo zikilinganishwa na mawazo yetu halisi kuhusu Mungu. Mtazamo halisi tulionao juu ya Mungu unaweza kuwa umezikwa chini ya takataka za itikadi za kawaida za kidini na unaweza kuhitaji uchunguzi makini na wa kina kabla haujafukuliwa na kufichuliwa wazi kama ulivyo. Ni pale tu tunapopitia nyakati za shida na uchungu ndipo tunaweza kugundua kile tunachoamini hasa kumhusu Mungu.

 3 Page 77 Mifano ya rejea

~ A. W. Tozer. The Knowledge of the Holy . New York: Harper San Francisco, 1961. uk. 2.

Mtu anaweza kujua mengi juu ya Mungu bila kumjua sana. Nina hakika kwamba wengi wetu hatujawahi kulielewa hili. Tunapata ndani yetu shauku kubwa katika theolojia (ambayo, bila shaka, ni elimu ya kuvutia zaidi – katika karne ya kumi na saba ilikuwa ni jambo ambalo kila mwanaume mstaarabu alilipenda). Tunasoma vitabu vya ufafanuzi na utetezi wa kitheolojia. Tunatazama katika historia ya Kikristo

Made with FlippingBook - Share PDF online