Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

2 9 2 /

M U N G U B A B A

maneno mengine, wa elimu ya kibiblia na kitheolojia kuhusu Utatu. Zingatia mambo makuu ya fundisho la Utatu: umoja wa Mungu, nafsi tatu zinazoshiriki asili moja katika Uungu, utofauti wa washiriki wa Utatu. Kwa kuzingatia mambo makuu unaweza kuweka mfumo ambao si tu kwamba utawasaidia wanafunzi kufahamu taarifa hizi, lakini pia utawapa njia ya kujifunza somo hili muhimu katika siku zijazo. Kujifunza ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi katika kipindi kimoja ni ama jambo la kimapinduzi au jambo la kijinga, au vyote viwili! Hakuna namna yoyote ambayo sehemu ya pili ya video, ambayo ilikusudiwa kuelezea kwa dakika thelathini muhtasari wa sifa kuu za Mungu wetu, ingeweza kwenda kwa kina na kuzifunua kikamilifu kweli hizi kuu. Kusudi la sehemu hii ni kuonyesha ukuu wa Baba yetu, na kupitia hilo, tuweze kuchochewa kumsifu na kumwabudu kwa maisha yetu. Mwitikio wetu kwa habari ya ukuu wa Bwana unapaswa kuwa ibada, utii wetu na kicho. Zab. 145:3 – “Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani.” Zab. 48:1 – “Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.” Zab. 96:4 – “Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.” Zab. 147:5 – “Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.” Ufu. 15:3 – “Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.” Zab. 147:5 – “Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka. Unapojadili na wanafunzi dhana ya ukuu wa Mungu na kufundisha mawazo yote muhimu, hakikisha unasisitiza wazo hili la ukuu. Pia, wapeleke wanafunzi kwenye

 5 Page 101 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook - Share PDF online