Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 2 9 3
M U N G U B A B A
kiambatisho cha Majina ya Mungu maana kinaangazia kwa njia tofauti asili ya utukufu wa Baba mwenye kupendeza na wa utukufu usio na kikomo. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa sifa mbalimbali na wanaweza kutoa maelezo kwa lugha ya kawaida kuhusiana na sifa hizi za Mungu.
Mifano hii halisi imekusudiwa kuchunguza umuhimu wa imani katika Mungu kama Utatu kwa ajili ya maisha na huduma. Wasaidie wanafunzi wafikirie kile kilicho hatarini katika kukana ukweli wa Maandiko kuhusu nafsi ya Mungu, na uwasaidie kufafanua mipaka ya kile kinachoonwa kuwa kinakubalika kwa habari ya maoni mbalimbali kuhusu Utatu. Kufikia mwisho wa somo la pili, unapaswa kuwa umewaeleza wanafunzi hitaji la wao kuwa wamefikiria na kufanya kazi ya msingi kwa ajili ya Kazi ya Huduma kwa Vitendo. Sasa, kufikia mwisho wa somo la tatu, unapaswa pia kuwa umesisitiza haja ya wao kuchagua kifungu kwa ajili ya Kazi yao ya Uchambuzi wa Maandiko (eksejesia). Kazi hizi zote mbili zina kawaida ya kuwashitukiza wanafunzi mwishoni mwa kozi, kwa hiyo hakikisha unawasisitiza kuhusu kazi zinazopaswa kufanywa, viwango vya kuzingatia wanapozifanya, na tarehe ambayo kazi zinatarajiwa kukamilika. Wape taarifa stahiki kuhusu kazi zao za mwisho na kazi nyingine zozote husika, na uwasihi wajipange na kuwa tayari kwa kazi hiyo kubwa iliyo mbele yao. Usiache kusisitiza mambo haya kwa wanafunzi wako kwani, katika masomo yoyote, mwisho wa kozi unashughuli nyingi, huku mambo mengi yakitarajiwa na wanafunzi huhisi shinikizo la kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ili kuendana na tarehe za kukamilisha mambo yote. Njia yoyote ambayo unaweza kutumia kuwakumbusha juu ya hitaji la kujipanga mapema itakuwa ya manufaa kwao, kwamba watalitambua hilo mara moja au la. Kwa sababu hii, tunashauri kwamba ufikirie kukata maksi kadhaa kwenye kazi zitakazokusanywa kwa kuchelewa. Ingawa kiwango cha maksi za kukatwa kinaweza kuwa cha kawaida, utekelezaji wako wa kanuni ulizojiwekea utawasaidia kujifunza kuwa makini, wenye ufanisi na kujali muda wakati wanapoendelea na masomo yao.
6 Page 105 Uchunguzi Kifani (Mifano Halisi)
7 Page 108 Kazi
Made with FlippingBook - Share PDF online