Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 2 9 5
M U N G U B A B A
Mungu kama Baba Wema wa Mungu
MAELEZO YA MKUFUNZI 4
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 4, Mungu kama Baba: Wema wa Mungu. Lengo la jumla la moduli ya Mungu Baba ni kuelewa katika sehemu ya kwanza maajabu na baraka mbalimbali za wema wa Mungu kwetu. Katika namna iliyo kinyume kabisa na ufafanuzi wa dhana ya Kiyunani ya “wema” kama aina ya ubora wa kimaadili, mtazamo wa kibiblia umetokana na ufunuo binafsi wa Mungu mwenyewe kama mwenye fadhili na neema, na ambaye kwa hakika huonyesha wema huo kwa viumbe vyote. Maandiko yanathibitisha kwa moyo wote kwamba YHWH ni mwema na anateda mema kwa ulimwengu wake wote, (1 Nya. 16:34; Zab. 119:68). Wema wa Bwana unahusishwa na jina lake lenyewe, (Zab. 52:9), ahadi zake zote, (Yos. 21:45), amri zake na neema na karama zake (Zab. 119:39; Rum. 7:12; Yak. 1:17), na kazi zake zote anapotengeneza na kusimamia historia yote kwa makusudi yake mwenyewe (Mwa. 50:20; Rum. 8:28). Uumbaji wenyewe ulifanywa katika mwanga wa wema yake (Mwa. 1:31), na katika matendo yake yote makuu ya ukombozi na wokovu anajithibitisha kuwa mwema kwa watu wake, Kwa mfano, alikuwa mwema katika ukombozi wake kwa Israeli kutoka Misri (Kut. 18:9), na mwema katika kuwarejesha kwake mwenyewe baada ya kurudi kwa mabaki kutoka utumwani (Ezra 7:9). Zaidi ya hayo, wema wa Mungu ni jambo la asili yake kabisa, ukionyweshwa katika ukombozi wake kwa watakatifu wake (Zab. 34:8), kwa wokovu hasa anaotoa kwa wale wanaomwamini (Flp. 1:6). Katika uhalisia, Mungu pekee ndiye anayeweza kutajwa kuwa mwema kweli (Zab. 14:1, 3; Mk 10:18). Katika sehemu hii, nia yetu ni kuwapa wanafunzi muhtasari wa utendaji wa ufahamu wa kibiblia kuhusu wema wa ajabu wa Mungu unaoonyeshwa katika sifa zake za kimaadili za usafi wake mkamilifu, uadilifu na ukamilifu, na upendo usio na mipaka. Wema wa usafi wa Mungu unaonyeshwa kupitia utakatifu wake, haki, na hukumu zenye adili, huku wema wa uadilifu na ukamilifu wake ukionyeshwa katika unyoofu wake, ukweli na uaminifu. Hatimaye, tutaona jinsi wema wa upendo wake wa milele unavyoonekana katika ukarimu, neema, rehema, na ustahimilivu wake. Katika sehemu ya pili tutaangalia ukali wa Mungu tukilinganisha na wema wake. Tutachunguza ghadhabu ya Mungu dhidi ya uasi na uovu wote. Katika Agano la Kale; ghadhabu ya Mungu inadhihirishwa dhidi ya dhambi na ukosefu wa haki (Hes. 11:10), dhidi ya ibada ya sanamu (Zab. 78:56-66), na dhidi ya wale wanaokataa na kupinga mapenzi yake mema, makamilifu, na ya kupendeza (Kum. 1:26-46; Yos. 7:1; Zab. 2:1-6). Siku bado inakuja ambapo Bwana ataonyesha, kwa
1 Page 111 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online