Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

2 9 6 /

M U N G U B A B A

namna ya uharibifu mkuu, ghadhabu yake itakayoachiliwa juu ya ulimwengu. Siku hiyo inaitwa “Siku Kuu ya Bwana” ( rej . Sef. 1:14-15; Isa. 13:9). Katika Agano Jipya, Yesu anathibitisha tena matazamio ya Mungu Baba Mwenyezi akimimina ghadhabu yake juu ya wale wanaokataa mapenzi yake ( rej. Lk 16:19-31). Matokeo ya kukataa maarifa ya Mungu ni makubwa na ya kutisha (Lk 13:3, 5; Yoh. 15:1-11; Mt. 3:7). Imani katika Yesu Kristo humwepusha mwamini na matokeo ya hakika ya kukumbwa na ghadhabu ya Mungu kwa wale wanaokataa zawadi ya Mungu katika Yeye (1 Thes. 1:10; Rum. 1:18-32; Efe. 2:2). Namna pekee inayoweza kufikirika ya kuelewa wema na ukali wa Mungu ni kuvielewa kwa pamoja. Kwa maneno mengine, jaribio lolote la kumwelezea au kumtafsiri Mungu kwa sifa moja au nyingine kati ya hizo ni aina ya fikra hasi ambazo hata Biblia yenyewe inakataa. Katika sehemu ya kwanza tutachunguza wema wa Mungu, na katika sehemu inayofuata tutatafakari ghadhabu ya Mungu. Iwapo kutakuwa na mkanganyiko au mvutano wowote katika somo letu, uwe na uhakika itakuwa katika kutoweza kwetu kuyaelewa pamoja na kwa wakati mmoja , na si katika udhihirisho halisi wa ukamilifu wa Mungu kama Mungu na mfalme wetu. Kwa mara nyingine, tafadhali angalia malengo. Kama kawaida, jukumu lako kama mkufunzi ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na katika kipindi chote uwapo pamoja na wanafunzi. Kadri unavyoweza kuangazia malengo katika muda wote wa kipindi, ndivyo utakavyoongeza zaidi uwezekano wa wao kuyaelewa malengo husika katika upana na kina chake. Inaonekana kuna ugonjwa kwa wale wanaosoma sifa za Mungu, ambao huelekea kumwambukiza karibu kila mfafanuzi wa Maandiko kama hatakuwa mwangalifu kuuona. Ni ugonjwa gani? Wafasiri wengi wa sifa za Mungu huwa wanasisitiza sifa moja ya Mungu huku wakiitenga na nyingine au kutoitilia mkazo kama nyingine. Aina hii ya usomaji, kulingana na ufahamu wangu, imejengwa katika wazo la kutazama tabia nzuri ya Mungu isiyo na kikomo kama vipengele . Ingawa, kwa faida ya kujifunza na uchambuzi, tunaweza kuzungumza juu ya sifa za Mungu kama orodha au mkusanyiko wa sifa za ukamilifu, ukweli ni kwamba Mungu hawezi kuunganishwa katika vipengele. Mungu anapotenda, Yeye hutenda kwa umoja na ukamilifu wake na bila mkanganyiko wala mgongano wowote katika sifa zake mwenyewe. Uhalisia wa alivyo, ni kama lile vazi la Bwana wetu lisilo

 2 Page 111 Ibada

Made with FlippingBook - Share PDF online