Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 2 9 7

M U N G U B A B A

na mshono; hakuna vipengele, vipande au migawanyiko katika tabia yake kuu. Mungu anapofanya kazi, kazi zake zinapatana kikamilifu na mapenzi yake na nafsi yake. Yeye ni Bwana. Kwa kutoweza kumtazama Mungu kama umoja, tunatenga sehemu ya sifa zake na kisha kusema kwa mamlaka juu ya sehemu hiyo bila kurejelea sifa zingine kuu zinazounda haiba yake. Matokeo yake mara nyingi ni mtazamo uliopotoka na usio wa kibiblia juu ya Mungu ambao unaleta mivutano ya uongo na isiyo ya lazima katika fikra zetu juu ya Mungu, mivutano na mikanganyiko ambayo kimsingi haipo na haipaswi kuwepo. Changamoto kwa kila mwanafunzi wa kweli wa Mungu ni kukuza ufahamu wa kwamba, linapokuja suala la elimu kuhusu Baba (au, kwa hakika, mshiriki yeyote wa Utatu) uchanganuzi si nafsi husika. Ingawa tunaweza kumchanganua Mungu kupitia sifa zake, hatupaswi kufikiri kwamba Mungu anaweza kugawanywa na kuchambuliwa kama riwaya au injini ya gari. Kama Bwana Aliye Hai, aliyetajwa na sifa zisizohesabika zinazoonyesha ukuu na wema wake, Yeye hutenda kama umoja, akiishi katika nafsi tatu, na kufanya mapenzi yake kwa ajili ya makusudi yake mwenyewe, kwa hekima kamilifu na subira. Tusifikiri kamwe katika kiburi chetu kwamba ni lazima Mungu alingane na chambuzi zetu. Badala yake, Mungu na atupe neema tusipumbazwe, wala kujidanganya wenyewe katika kujifanya kwamba Mungu anapaswa kulingana na akili zetu. Asili ya akili ovu ni kujifanya kana kwamba Mungu anatenda na kuwaza kama zenyewe (rej. Zab. 50:21 – “Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.” Mpe Mungu nafasi ya kukushangaza kwa mafunuo yake mapya ya ujumla wa vile alivyo, na si tu sehemu moja unayovutiwa nayo. Yeye ni Bwana! Mchakato wako wa kupitia sifa hizi zinazohusiana na wema wa Mungu unapaswa kulingana na ulichofanya katika kupitia sifa za ukuu wa Mungu. Kwa maneno mengine, lengo la sehemu hii ni kutoa muhtasari ambao wanafunzi wanaweza kuutumia ili kupata “mtazamo wa jicho la ndege” wa ufahamu wa kitaaluma kuhusu wema wa Mungu. Utajiri na kina ambacho kila moja ya sifa inadai, uangalifu na umakini unaohitajika, haviwezi kutolewa hapa. Kinachoweza kufanyika, hata

 3 Page 115

Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook - Share PDF online