Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

2 9 8 /

M U N G U B A B A

hivyo, ni kutafuta kuwawezesha wanafunzi kuelewa picha ya jumla ya majadiliano ya kitheolojia kuhusu sifa za kiadili za Mungu, na kutengeneza ramani kwa ajili ya utafiti wao wa baadaye. Tafadhali hakikisha kwamba unawatahadharisha wanafunzi wako kuhusu lengo la sehemu hii, na dhamira ya maudhui ya sehemu hii.

Unapojibu maswali haya hakikisha kwamba 1) unakumbuka kuwa lengo hapa ni kuwasaidia kupitia upya mambo makuu yanayohusiana na sehemu ya kwanza ya video na ufafanuzi wake wa muhtasari wa sifa za Mungu za kiadili, na 2) wanafunzi wanachanjwa dhidi ya maradhi ya kuzitazama sifa za Mungu moja moja huku wakizitenga na kupunguza msisitizo kwa nyingine. Wakumbushe umuhimu wa kujua kwamba ingawa kiakili tunaweza kuzingatia vipengele tofauti, kiuhalisia Mungu wetu mtukufu ni mmoja. Kum. 6:4 – Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Isa. 45:5-6 – Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua; 6 ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine. Wasihi wanafunzi kukumbuka kwamba Mungu ni mmoja na hutenda kwa uwiano katika sifa zake zote kwa wakati mmoja. Changamoto ya kulitetea wazo la ghadhabu ya Mungu tunapozingatia wema wake si jambo ambalo linahimizwa katika mazingira mengi ya kanisa leo. Kutokuwapo kwa mwelekeo huu kumetokeza kizazi cha Wakrsito ambao kitheolojia na kimaadili wametoka nje na kuiacha njia, wakiyumba-yumba maishani kwa sababu wanazingatia tu zile sifa zinazoonekana kuambatana na uzoefu wao na maslahi yao wenyewe, na taratibu wakizipa kisogo zile zisizoendana na matakwa yao. Jambo kuu katika kujadili hili na wanafunzi ni kupinga moja kwa moja dhana ya “haki” yao ya kuchambua na kuchagua ni sifa gani za Mungu wanazotaka kuzizingatia na kusisitiza. Hakuna Mkristo aliye na haki ya kuchanganua Biblia, akiruka na kuzama kwenye maandiko yanayofaa kwa mtazamo wake, huku akishindana na kupuuza kwa makusudi “maneno magumu” ya Biblia.

 4 Page 130 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu

 5 Page 140 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook - Share PDF online