Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 2 9 9
M U N G U B A B A
Unapopitia maswali haya ya mwisho, hakikisha kwamba unawakumbusha wanafunzi juu ya hitaji hili lililopo kila wakati la kupokea ufunuo wa Mungu kama anavyoutoa, na sio kama tunavyotaka kuusikia. Kumbuka kemeo la Yesu kwa Petro uko Kaisaria Filipi: Mt. 16:21-23 – Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. 22 Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. 23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. Kupitia mifano halisi katika somo hili, jaribu kuwasaidia wanafunzi kukabiliana na dhana ya ghadhabu ya Mungu na njia mbalimbali ambazo watu ulimwenguni na Kanisa leo wanafikiria. Wanapojifunza zaidi na zaidi yale ambayo Maandiko yanafundisha juu ya nafsi ya Mungu Baba Mwenyezi, itawabidi watumie uwezo wao wa kujihusisha na kukanusha mawazo mbalimbali kuhusu Mungu ambayo hayapatani na ufunuo wake mwenyewe katika Maandiko. Ingawa tabia ya kudhani kwamba Fundisho kuhusu Mungu si la kivitendo ipo kwa wengi, hilo si kweli hata kidogo. Mifano hii halisi ilikusanywa ili kuwasaidia wanafunzi wako waweze kuielewa mitazamo ya kisasa kuhusu Mungu na ghadabu yake, na jinsi wanavyoshughulikia maswali na majibu wanayotoa itakuwa na athari kubwa kwa matokeo ya huduma zao katika siku zijazo. Hongera, umefundisha modui ya Mungu Baba, lakini bado haujamaliza kazi yako! Kazi yako kama mkufunzi na mtayarishaji wa maksi na viwango vya ufaulu inaanza sasa. Hakikisha kwamba umewapa wanafunzi taarifa zote zinazohitajika kuhusu tarehe na kazi za kukusanya, na kwamba umepata kutoka kwao mapendekezo yao kuhusu Kazi ya Huduma kwa Vitendo na Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko, pamoja na taarifa nyingine yoyote ambayo itakuwa muhimu kwako katika kuamua daraja la jumla la mwanafunzi. Mara nyingine tena, busara yako kuhusu kazi
6 Page 142 Mifano Halisi
7 Page 145 Kazi
Made with FlippingBook - Share PDF online