Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

3 8 /

M U N G U B A B A

Mungu Asiyekuwepo

Kwa sababu ya ongezeko kubwa la vurugu na uhalifu katika jamii, kanisa lako linaandaa mkutano wa maombi kwa ajili ya wanajamii. Likiwa limepanga matembezi na mikesha ya maombi, kusanyiko la kanisa lako linafahamu kwa kina kuhusu nguvu za kiroho zinazosababisha vurugu na ukatili unaoendelea mtaani. Katika moja ya vipindi vya maombi, mkazi mmoja ambaye si sehemu ya kanisa lako anasimama na kusema, “Mimi si mshirika wa kanisa hili, na kusema kweli, siendi kanisa lolote kwa sababu Mungu anaonekana kutotujali kama anavyowajali wengine. Kwa nini mitaa yetu mara zote lazima iwe na hofu na huzuni? Anaonekana kujali zaidi watu waishio kwenye vitongoji vya matajiri kuliko sisi hapa. Anaonekana hayupo sana hapa!” Mkutano mzima wa maombi unanyamazishwa, na kukugeukia ili ujibu kilio cha moyo wa jirani huyu anayeonekana kuchanganyikiwa. Ni ufafanuzi na maneno gani ya faraja ungeweza kutoa katika mkutano wa maombi kuhusu hoja hii? Mabishano yamekuwa yakiibuka kwa muda mrefu miongoni mwa washirika wa kanisa lako la mahali kwa sababu ya msisitizo mpya kuhusu “sifa na kuabudu kama jambo binafsi na la ndani kabisa.” Akiwa amechoshwa na hali ya zamani ya uimbaji wa nyimbo na liturujia za kale, kiongozi mpya wa ibada amekuwa akiingiza katika utaratibu wa huduma nyimbo mpya za sifa na kuabudu, ambazo nyingi ya hizo zinamzungumzia Mungu kwa maneno ya uhusiano wa ndani sana, wa kibinafsi. Baadhi ya waumini wa muda mrefu wanapinga, wakihisi kwamba muziki na msisitizo mpya unamfanya Mungu aonekane kuwa wa karibu zaidi, na ile hofu ya Mungu kama aliye mkamilifu kuliko sisi imeondoka kabisa. Hofu yao kubwa ni kwamba ile nafasi ya kicho na hofu ya Mungu imechukuliwa na dhana ya Bwana ambaye ni rafiki yangu. Nani yuko sahihi na nani ana makosa hapa? Je mitazamo yote miwili inaweza kuwa sawa na si sawa kwa wakati mmoja ? Kivipi? Kama ungekuwa kiongozi wa kanisa hili, ungewezaje kuzisaidia pande zote mbili kuelewa jinsi uwepo wa Mungu katika uumbaji wake na sifa yake ya kuwa juu zaidi ya vyote vinavyoboresha uzoefu wetu wa ibada kwa Mungu? Prolegomena, elimu ya “mambo ya kwanza” ya Fundisho la Mungu, huthibitisha kwa unyenyekevu kwamba kabla hatujamjua Mungu ni lazima ajifunue mwenyewe kwetu. Mungu amejifunua kwetu kwa namna mbili maalum. Katika ufunuo wa jumla, Mungu amejifunua kwa watu wote kila mahali, na katika ufunuo maalum, Mungu hujifunua kwa watu maalum kwa wakati na mahali maalum. Katika uhusiano wake na ulimwengu aliouumba, Mungu yupo katikati ya uumbaji na yuko juu zaidi ya Bwana Ambaye ni Rafiki Yangu

2

1

3

Marudio ya Tasnifu ya Somo

Made with FlippingBook - Share PDF online