Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 3 9
M U N G U B A B A
uumbaji. Uwepo wa Mungu katikati ya uumbaji unarejelea uhusika wake wa sasa na hai katika uumbaji wake wote; wakati sifa yake kama aliye juu zaidi ya uumbaji inarejelea ukweli kwamba Mungu hana ukomo na kwa sababu hiyo hawezi kutoshea katika uumbaji wake au kujulikana pasipo uchaguzi wake mkuu wa kujifunua kwetu. Sifa za Mungu zinarejelea tabia za Utatu wote wa Mungu kwa ujumla, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, na zinaweza kugawanywa kwa misingi ya ukuu wake na wema wake. Sifa za ukuu wake zinahusisha hali yake ya kiroho, uzima, haiba, kutokuwa na ukomo, na kudumu huku sifa za wema wake zikihusisha utakatifu, ukamilifu, na upendo wake. Ikiwa una nia ya kuendelea kufuatilia baadhi ya mawazo ya Prolegomena: Fundisho kuhusu Mungu na Kuenea kwa Ufalme, unaweza kujaribu vitabu hivi: Evans, William. The Great Doctrines of the Bible. Chicago: Moody Press, 1976. Schaeffer, Francis A. The God Who is There. Chicago: InterVarsity Press, 1968. Stone, Nathan J. Names of God. Chicago: Moody Press, 1993. Sasa ni wakati wa wewe kufikiria kwa vitendo kuhusu maana ya kweli hizi kwa maisha yako binafsi na huduma. Zingatia hali ya maisha yako leo, na ufikirie juu ya njia ambayo Roho Mtakatifu anaweza kukutaka uhusishe kweli hizi kuhusu asili na vile Mungu alivyo kwa kile unachofanya sasa hivi. Ahadi ya Yakobo katika Waraka wa Yakobo 1:22-25 ni kwamba Baraka maalum kabisa huwajia wale ambao si wasikiaji tu wa Neno la Mungu bali watendaji wake. Tafakari juu ya kile hasa ambacho Roho Mtakatifu anakipendekeza kwako ukizingatie juma hili kuhusiana na ufunuo wa jumla na ufunuo maalum wa Mungu, uwepo wake katikati ya uumbaji wake na sifa yake kama aliyejuu zaidi ya uumbaji wake, na maana ya kweli hizi kuu kwa kile ambacho Mungu anakuitia kukifanya leo? Ni mtu gani hasa, tukio, au hali inayokuja akilini kwa ajili ya kuzingatia kwako mwenyewenamatumizi yakweli hizi juuyaFundishokuhusuMunguunapozitafakari? Je, kuna eneo katika maisha na huduma yako ambalo linahitaji matumizi yako ya sasa ya kweli hizi? Ikiwa ndivyo, Mungu anataka ufanye nini kuhusiana na maeneo hayo? Je, kuna mtu katika huduma yako ambaye unadhani anahitaji kuelewa na kutumia mafundisho ya Neno la Mungu katika maeneo hayo maishani mwake? Utawasilishaje somo hili kwake? Ni wakati au mazingira gani mazuri ya kumshirikisha ufahamu wako?
1
Nyenzo na Bibliografia
Kuhusianisha somo na huduma
Made with FlippingBook - Share PDF online