Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 6 1

M U N G U B A B A

B. Umuhimu wa utawala wa Mungu juu ya ulimwengu

1. Je, Mungu ndiye mwanzilishi wa uovu na dhambi? ?

a. Hapana! Chanzo cha machafuko na uharibifu ulimwenguni ni uasi wa shetani na wanadamu ambao wameukataa utawala wa ufalme wa Mungu (Mungu si mwanzilishi wa dhambi, rej. Yakobo).

b. Shida na ukatili ulimwenguni vinatokana na tamaa, ubinafsi, na kiburi cha mfumo wa ulimwengu na wale waliomo, 1 Yohana 2:15-17.

2

c. Mambo yaliyokusudiwa kwa ajili ya uovu, Mungu anaweza kuyatumia kwa ajili ya wema wa kusudi lake mwenyewe. (1) Utumwa wa Yusufu, Mwa. 50:20 (2) Kifo cha Yesu, Mdo 2:23

2. Kama Mungu si mwanzilishi wa uovu na dhambi, kwa nini ameruhusu au huruhusu viwepo?

a. Mapenzi ya Mungu yanapita uelewa wetu wa nini kimeruhusiwa na/au nini kimekataliwa. Kama Mungu mwenye enzi, hufanya mambo yote sawa na mapenzi yake mwenyewe. (1) Vitu vyote vina mwanzo, utegemezi, na mwisho katika Mungu, Rum. 11:36. (2) Vitu vyote vimefanywa kwa utukufu wa Mungu, Mit. 16:4.

b. Namna anavyozitumia nyakati na njia zake za utendaji vimetoa nafasi kwa uovu kuwepo hadi atakapoamua mwisho wake. (1) Bwana huweka mipaka juu ya mateso na uovu, 2 Pet. 2:9.

Made with FlippingBook - Share PDF online