Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 6 7
M U N G U B A B A
³ Bila kujali nadharia zinazotolewa kuhusu chimbuko la ulimwengu, hakuna mtu na hakuna kitu kinachoweza kudai kwa namna yoyote kuwa na uwezo wa kujitegemea mbali na Mungu aliye chanzo cha viumbe vyote. ³ Uelewa sahihi wa uangalizi na utunzaji wa Mungu hutatua baadhi ya makosa ya kisasa ya falsafa na theolojia, kama vile pantheism, deism, falsafa ya jaala (fatalism), na ile ya bahati (chance). Wazo la utawala wa Mungu lina maana na umuhimu wa moja kwa moja kwa yote ambayo utapata kuyatenda katika huduma kwa ajili ya Bwana. Hii ni fursa yako ya kufanya mjadala na kikundi chako kuhusu masuala na maeneo ambayo yanahusiana moja kwa moja na maslahi yako, maswali yako na hali yako. Ili kuhudumia wengine kwa ufanisi, lazima uweze kuainisha kanuni za Maandiko na kuhusianisha kweli zake na maisha yako mwenyewe kwanza. Ni maswali gani maalum yanayokuja akilini na rohoni mwako baada ya kujifunza kweli hizi kuhusu utunzaji, uhifadhi, na utawala wa Mungu? Maswali yaliyo hapa chini yanalenga kuibua maswali yako mwenyewe ambayo ni muhimu zaidi na mahususi zaidi. * Tunajua kwamba Mungu “hana upendeleo” (rej. Yakobo 2:1), lakini kwa kutazama kwa haraka inaonekana kama miji yetu inakumbana na sehemu kubwa ya taabu na ukatili wa maisha haya. Je, unaweza kuelezea hili katika mwanga wa utunzaji na uangalizi wa Mungu juu ya vitu vyote? * Watu wengi huwalaumu maskini kwa nyakati zao ngumu na taabu wanazopitia. Je, tunapaswa kuelewa vipi mahangaiko yao katika mwanga wa fundisho la uangalizi na utunzaji wa Mungu? * Kwa nini Mungu hakukomesha dhambi zote na laana katika kifo cha Yesu? Kwa nini anatoa uhuru wowote kwa shetani na kazi yake duniani? * Je, tunawezaje kusemaje kwa ujasiri wa mioyo yetu yote kwamba ingawa Mungu ndiye anayeongoza vitu vyote, yeye si mwanzilishi wa kifo, uharibifu, na ukatili ambao umeenea katika ulimwengu leo? * Kwa kuzingatia ufahamu tulio nao kwamba Mungu si mwanzilishi wa uovu na dhambi na wala hataki vitokee, tunapaswa kuwa na mwitikio gani tunapokabiliana na mambo hayo?
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
2
Made with FlippingBook - Share PDF online