Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

6 6 /

M U N G U B A B A

8. Ni kwa namna gani fundisho la uhifadhi wa Mungu na utawala wake linatatua makosa ya pantheism? Unawezaje kujibu madai ya deism kwamba Mungu hayupo katika mambo ya uumbaji wala hahusiki nayo? Ni kwa namna gani ukweli kwamba Mungu huhifadhi na kusimamia vitu vyote unatatua makosa ya falsafa ya jaala (fatalism) na determinism?

MUUNGANIKO

Somo hili linaangazia fundisho la Mungu kama mtunzaji, Bwana Mwenye enzi ambaye ni Chanzo na mtegemezaji wa vitu vyote, akivihifadhi na kuvisimamia vyote katika hekima yake. Vitu vyote vipo kwa sababu ya mapenzi yake Yeye aliye Muumba wa vyote, na vyote vitaleta utukufu kwa Jina lake, jambo ambalo ndilo kusudi hasa linalounganisha uhai wa vitu vyote kila mahali. ³ Uumbaji wote na historia vinadhihirisha kwamba Mungu anayo mamlaka kuu na utawala juu ya vyote. ³ “Uangalizi na Utunzaji wa Mungu” unarejelea ukweli kwamba “Mungu hutimiza mapenzi yake makuu ulimwenguni ambamo matukio yote yamepangwa na yeye kwa ajili ya kutimiza kusudi lake jema kwa ajili yake na uumbaji.” ³ Maandiko yanatufundisha kwamba Baba Mwenyezi ni mwenye enzi juu ya vyote, Chanzo cha yote, na Mtegemezaji wa yote kupitia Mwanawe, Yesu Kristo. Mambo yote yamewekwa ili kuendana na mapenzi yake kwa ajili yake mwenyewe, ili ajitwalie utukufu kwa vitu vyote. ³ Mungu amedhihirisha utawala wake mkuu juu ya yote kupitia uhifadhi na usimamizi wake wa vitu vyote. ³ “Uhifadhi” unarejelea ukweli kwamba vitu vyote vipo na vimeshikamana pamoja kwa uweza wa utunzaji na ufadhili wa Mungu, na “utawala” unarejelea ukweli kwamba Mungu ni mkuu na mwenye enzi juu ya ulimwengu wote, anayo mamlaka yote ya kufanya lolote analokusudia katika uumbaji wake. ³ Kama ategemezaye vitu vyote kupitia Yesu Kristo, Mungu atazidhihirisha mbingu mpya na nchi mpya katika urejesho wa vitu vyote wakati wa ujio wa Pili wa Kristo.

Muhtasari wa Dhana Muhimu

2

Made with FlippingBook - Share PDF online