Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 6 5
M U N G U B A B A
Hitimisho
» Kazi maalum ya uangalizi na utunzaji wa Mungu inafunuliwa kupitia uhifadhi na utawala wake wa vitu vyote. » Mungu wetu si tu kwamba aliumba vitu vyote, lakini huvitunza kwa nguvu zake na kuvitawala kwa hekima yake, vyote kwa utuku wake mwenyewe.
Jibu maswali yafuatayo ambayo yatakusaidia kufikiri upya maudhui ya video ya sehemu ya pili ambayo umeitazama na umuhimu wake. Bila shaka, tunahitaji kuwa na muda wa kutafakari kwa kina na wa maombi ili kuweza kuelewa namna ambavyo Mungu kama Bwana mwenye mamlaka juu ya ulimwengu anavyohusiana na mfumo wa ulimwengu uliojaa kila aina ya uovu, usumbufu, machafuko na ukatili. Jitaidi kujibu kwa ukamilifu na uwazi, na mara zote, kama kawaida, jenga hoja zako kwa uthibitisho wa Maandiko! 1. Nini maana ya neno la kitheolojia “uhifadhi wa Mungu”? Kwa nini haiwezekani kuthibitisha kwamba kitu chochote katika ulimwengu kinaweza kujitegemeza kwa kusudi lake na nguvu zake binafsi? 2. Je, kuna kitu chochote katika uumbaji wote kinachoweza kudai kwamba kipo huru mbali na Mungu na nguvu zake? Elezea jibu lako. 3. Je, fundisho la uhifadhi wa Mungu lina umuhimu na matokeo gani kwa mjadala wa mageuzi? Sisi kama waamini tunapaswa kuwa na msimamo gani kuhusu uumbaji tuwapo katikati ya mijadala na mabishano ya aina hii? 4. Msemo huu wa kifundisho “utawala wa Mungu?” una maana gani? Pana uhusiano gani kati ya Mungu na mambo ya wanadamu na ya mataifa? 5. Kusudi moja la vitu vyote ulimwenguni ni lipi? Mungu amekusudia nini kuhusiana na uumbaji wakati wa Ujio wa Pili wa Yesu Kristo? 6. Je, Mungu ndiye mwanzilishi wa uovu na maafa duniani? Kama Mungu si mwanzilishi wa uovu, kwa nini basi anauruhusu? 7. Wanadamu wanawezaje kuwajibika kwa matendo yao ikiwa kweli Mungu ndiye mtawala wa vitu vyote vya mbinguni na vya duniani? Mungu anakusudi gani kuhusu hiari ya mwanadamu?
Sehemu ya 2
Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
2
page 282 6
Made with FlippingBook - Share PDF online