Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
8 8 /
M U N G U B A B A
3. Mtazamo huu haukuwahi kupata umaarufu katika Kanisa.
C. Nadharia ya “Modalistic Monarchianism”: Mungu mmoja akijidhihirisha katika namna tatu.
1. Kuna Uungu Mtakatifu mmoja unaoweza kutajwa kama Baba, Mwana, au Roho.
2. Majina haya hayaelezei tofauti dhahiri za washiriki au nafsi tofauti katika Uungu Mtakatifu.
3. Majina haya yanamrejelea Mungu mmoja atendaye kazi katika nyakati tofauti kwa namna tatu tofauti.
3
4. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni nafsi ileile itendayo kazi kwa njia tatu tofauti (nafsi moja ikiwa na majina, shughuli, au majukumu matatu tofauti).
5. Mtazamo huu hauwezi kuelezea kikamilifu kile ambacho Biblia inafundisha hasa kuhusu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
D. Muundo Halisi wa Kiimani (Mtaguso wa Konstantinopoli [381] na mtazamo wa Athanasius [293-373] na mababa wa Kapadokia [Basil, Gregory wa Nazianzus, na Gregory wa Nyssa])
1. Mungu ana kiini au dutu moja ( ousia ) ambayo ipo katika nafsi tatu (hypostases).
2. Mungu ana kiini au asili moja , lakini yuko katika nafsi tatu tofauti .
Made with FlippingBook - Share PDF online