Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 9 9

M U N G U B A B A

1. Mungu hana mipaka katika undani wake, na kwa hivyo yuko huru kufanya chochote anachotaka ndani ya kusudi na mapenzi yake mwenyewe.

2. Mungu hazuiliwi na wakati (muda) na mahali; yuko juu na zaidi ya vipengele hivyo, lakini anaweza kuvielewa na kuvitumia kwa makusudi yake.

3. Mungu huona vitu vyote katika muono sahihi, akiwa na uwezo wa kuzifikia kikamilifu taarifa zote kuhusu vitu vyote kwa wakati mmoja.

4. Mungu yuko huru kutimiza lolote na chochote kulingana na uradhi wa mapenzi yake mwenyewe, kwa sababu ya uwezo wake usio na kikomo, hekima yake, na asili yake.

3

V. Mungu Baba Mwenyezi Habadiliki (Anadumu).

A. Vipengele vya kudumu kwa Mungu

1. Mungu hataacha kuwa; atadumu zaidi ya yote na juu ya yote, Zab. 102:26-27.

2. Bwana habadiliki; alivyo, ndivyo ambavyo amekua na atakuwa daima.

a. Mal. 3:6

b. Hes. 23:19

Made with FlippingBook - Share PDF online