Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
1 0 /
M U N G U B A B A
Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Zoezi hili linawakilisha sehemu muhimu ya ushiriki wako katika moduli ya Mungu Baba . Ili kutimiza takwa hili, unatakiwa uchague kifungu cha Maandiko , na ufanye utafiti na ufafanuzi wa kina ( eksejesia ) wa andiko husika. Unaweza kuchagua mojawapo ya maandiko yafuatayo: Matendo 17:24-31 Isaya 40:22-26 Warumi 9:13-18 Danieli 4:34-37 Psalms 103.9-18 Mathayo 6:25-33 Zaburi 104:24-30 Kusudi la kazi hii ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa kifungu muhimu juu ya somo la utunzaji na usimamizi wa Mungu, uhifadhi na utawala wake juu ya viumbe vyote, na maana ya hayo kwa maisha yetu leo. Pengine hakuna kitu muhimu zaidi kwa kiongozi wa Kikristo kuliko uwezo wake wa kufafanua maana ya Maandiko, na kuihusisha na masuala halisi ya maisha ya watu leo. Lengo sio tu uweze kufafanua maana ya kifungu, lakini pia kuhusisha maana hiyo moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, na maisha ya wale ambao Mungu amekuita kuwahudumia ndani na kupitia kanisa lako au huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia , ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika ? Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)
Dhumuni
Mpangilio na muundo
Made with FlippingBook - Online catalogs