Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
This is the Swahili edition of Capstone Module 6: God the Father.
Jiwe Walilolikataa Waashi Limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni
THE UR BAN
Mungu Baba
MI N I S T R Y I NS T I TUT E h u d uma y a WOR L D IMPAC T , I NC .
u
b
c
a
h
i t
a
K
M
i
z
w
n
a
u
f
n
a
Moduli ya 6 Theolojia & Maadili
SWAHILI
K I T A B U C H A M W A N A F U N Z I
Mungu Baba
Moduli ya 6
Theolojia na Maadili
Prolegomena:
FUNDISHO KUHUSU MUNGU na KUENEA KWA UFALME
Mungu kama Muumba:
UANGALIZI NA UTUNZAJI WA MUNGU
Mungu katika Utatu:
UKUU WA MUNGU
Mungu kama Baba:
WEMA WA MUNGU
Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia vitabu hivi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .
Moduli ya 6 ya Mataala wa Capstone: Mungu Baba – Kitabu cha Mwanafunzi ISBN: 978-1-62932-376-3 © 2005, 2011, 2013, 2015. Taasisi ya The Urban Ministry Institute . Haki zote zimehifadhiwa. Toleo la Kwanza 2005, Toleo la Pili 2011, Toleo la Tatu 2013, Toleo la Nne 2015. © 2024 Toleo la Kiswahili, kimetafsiriwa na Mch. Samuel Gripper na Mch. Eresh Tchakubuta. Tunatambua na kuheshimu utumishi uliotukuka wa Mtume K. E. Kisart kwa kujitolea kwake bila kukatishwa tamaa kuwafundisha viongozi katika Injili. Hairuhusiwi kunakili, kusambaza na/au kuuza vitabu hivi, au matumizi mengine yoyote pasipo idhini, isipokuwa kwa matumizi yanayo ruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Haki Miliki ya Mwaka 1976 au kwa idhini ya maandishi kutoka kwa mmiliki. Maombi ya idhini yatumwe katika maandishi kwa taasisi ya: The Urban Ministry Institute , 3701 E. 13th Street, Wichita, KS 67208. Taasisi ya The Urban Ministry Institute ni huduma ya World Impact, Inc Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997, iliyochapishwa na The Bible Society of Tanzania . Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.
Yaliyomo
Muhtasari wa kozi
3 5 7
Kuhusu Mkufunzi
Utangulizi wa Moduli
Mahitaji ya Kozi
15
Somo la 1 Prolegomena: Fundisho kuhusu Mungu na Kuenea kwa Ufalme
1
47
Somo la 2 Mungu kama Muumba: Uangalizi na Utunzaji wa Mungu
2
85
Somo la 3 Mungu katika Utatu: Ukuu wa Mungu
3
125
Somo la 4 Mungu kama Baba: Wema wa Mungu
4
159
Viambatisho
/ 3
M U N G U B A B A
Kuhusu Mkufunzi
Mchungaji Dkt. Don L. Davis ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry Institute na ni Makamu wa kwanza wa Rais wa World Impact. Alisoma katika Chuo cha Wheaton College na Chuo cha Uzamili cha Wheaton na kuhitimu kwa ufaulu wa kiwango cha juu, yaani Summa Cum Claude, katika ngazi ya Shahada (1988) na Shahada ya Uzamili (1989) katika Masomo ya Biblia na Theolojia ya Utaratibu. Alipata Shahada yake ya Uzamivu katika Masuala ya Dini (Theolojia na Maadili) katika chuo kikuu cha Iowa School of Religion. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi na Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact , anasimamia mafunzo ya wamishenari wa mijini, wapanda makanisa, na wachungaji wa majiji, na kufanya uwezeshaji kupitia fursa za mafunzo kwa watendakazi Wakristo wa mijini katika uinjilisti, ukuaji wa kanisa, na umisheni wa upainia. Pia anaongoza Mpango wa Mafunzo huria kwa wale wanaosoma wakiwa mbali, vilevile anawezesha Mafunzo ya Kiuongozi kwa mashirika na madhehebu kadhaa kama Prison fellowship, The Evangelical Free Church of America na The Church of God in Christ. Dkt. Davis, ambaye ametunukiwa tuzo nyingi za ualimu na za kitaalamu, amewahi kuwa profesa na Mkuu wa vitivo katika taasisi kadhaa za kitaalamu zenye hadhi ya juu, baada ya kuhadhiri na kufundisha kozi za dini, theolojia, falsafa, na mafunzo ya Biblia katika taasisi za elimu ya juu kama vile Chuo cha Wheaton, Chuo Kikuu cha St. Ambrose, Programu ya Shahada ya Uzamili ya Theolojia ya Chuo Kikuu cha Houston, Kitengo cha Dini cha Chuo Kikuu cha Iowa, na Taasisi ya Mafunzo ya Ibada ya Robert E. Webber. Ameandika idadi kubwa ya vitabu, mitaala, na nyenzo za kujifunzia ili kuwaandaa viongozi wa mijini, ikijumuisha mtaala wa mafunzo wa Capstone (hii ni programu mama ya TUMI yenye moduli 16 za hadhi ya mafunzo ya seminari, yanayotolewa kupitia mfumo wa elimu ya masafa), Mizizi Mitakatifu: Kidokezo cha Namna ya Kurejesha Mapokeo Makuu , ambayo inaangazia namna makanisa ya mijini yanavyoweza kufanywa upya kupitia kugundua upya imani halisi, sahihi ya kihistoria; na Mweusi na Mwanadamu: Kumgundua Upya M.L. King kama Nyenzo ya Theolojia na Maadili ya Weusi . Dkt. Davis pia ameshiriki katika mihadhara ya kitaalamu kama the Staley Lecture series, makongamano ya kufanywa upya kama Promise Keeper Rallies na miungano ya kithiologia kama The University of Virginia Lived Theology Project Series. Vilevile alipokea tuzo ya heshima ya mwanafunzi mashuhuri ( Alumni Fellow Award ) kutoka Chuo Kikuu cha Iowa cha Sanaa na Sayansi za Kiliberali mnamo 2009. Dkt. Davis pia ni mwanachama wa The Society of Biblical Literature, na The American Academy of Religion .
/ 5
M U N G U B A B A
Utangulizi wa Moduli
Salamu, wapendwa marafiki, katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Somo la nafsi ya Mungu wetu, Baba Mwenyezi, ni moja ya masomo muhimu na ya thamani sana kuliko masomo yote katika Neno la Mungu. Somo hili linaathiri kila nyanja ya ufuasi wetu, ibada, na huduma; hakika, ni kama Bwana wetu Yesu alivyosema, “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma,” (Yohana 17:3). Katika somo letu la kwanza, Prolegomena: Fundisho kuhusu Mungu na Kuenea kwa Ufalme , tutachunguza kwa ufupi mambo ya kwanza, prolegomena , ambayo ni msingi wa theolojia, huku tukiangalia umuhimu wa Mungu kujifunua kwetu. Tutajifunza dhana za ufunuo wa jumla na ufunuo maalum, na kuchunguza kwa makini umuhimu wa kujifunza Fundisho kuhusu Mungu kwa msingi wa uwepo wake, yaani, ushiriki wake wa sasa na hai katika uumbaji, pamoja na umilele wake, asili yake isiyo na ukomo na kutojulikana kwake. Katika somo letu la pili, Mungu kama Muumba: Uangalizi na Utunzaji wa Mungu , tutachunguza ukuu wa mamlaka ya Mungu na uangalizi na utunzaji wake juu ya viumbe vyote na historia. Mungu hufanya mambo yote kulingana na mapenzi yake. Baba Mwenyezi ni mwenye enzi juu ya yote, chanzo cha uhai wote, na mtegemezaji wa yote kupitia Mwana wake, Yesu Kristo. Tutachunguza pia namna utawala wa Mungu unavyoonyeshwa katika uhifadhi na usimamizi wake kwa vitu vyote, na tutaona jinsi ufahamu thabiti wa Kibiblia kuhusu uangalizi na utunzaji wa Mungu unavyoweza kutatua makosa makubwa ya kisasa katika falsafa na theolojia, hususan imani kwamba Mungu ni sawa na uumbaji wake ( pantheism ), imani kwamba Mungu aliyeumba ulimwengu hajihusishi tena na mambo ya ulimwengu ( deism ), mtazamo kwamba matukio yote ya zamani, ya sasa na ya baadaye, yamepangwa tayari na Mungu na kwa sababu hiyo hayawezi kuepukika ( fatalism ), na msimamo kwamba mambo yote hutokea kwa bahati nasibu ( chance ). Tunabadili uelekeo kidogo katika somo letu la tatu, Mungu katika Utatu: Ukuu wa Mungu . Tutaangalia ushahidi wa Kibiblia kuhusu Utatu, Mungu katika nafsi tatu. Maandiko yanafundisha kwamba kuna Mungu mmoja tu, na Mungu huyu mmoja anajifunua kwetu kama Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Washirika wa Utatu wako katika hali ya umoja, utofauti na usawa, Mungu mmoja wa kweli, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Mara baada ya kuchunguza Utatu, sasa tutachunguza kwa ufupi sifa za ukuu wa Mungu: hali yake ya kiroho, uzima wake, haiba yake, hali yake ya kutokuwa na ukomo, na asili yake ya kutobadilika.
6 /
M U N G U B A B A
Hatimaye, katika somo la nne tunaelekeza mawazo yetu kwa Mungu kama Baba: Wema wa Mungu . Hapa tutautambua wema wa ajabu wa Mungu unaoonyeshwa katika sifa zake za usafi wa kiadili, ukamilifu wake usio na waha, na pendo lake lisilo na mipaka. Na tutahitimisha moduli yetu kwa kuangalia wema na ukali wa Mungu, tukichunguza uhusiano baina ya wema na ukali wa Mungu, upendo na haki yake. Hakika, Mungu wetu Baba Mwenyezi ndiye mmoja, wa kweli, na Mungu wa mbinguni mwenye utukufu. Kumjua kikamilifu kutatusaidia kumwakilisha kwa heshima kama watumishi wake. Mungu akubariki unapochunguza utajiri wa Maandiko usioelezeka kumhusu Mungu wetu mkuu.
- Mch. Dkt. Don L. Davis
/ 7
M U N G U B A B A
Mahitaji ya Kozi
• Biblia (kwa madhumuni ya kozi hii, Biblia yako inapaswa kuwa tafsiri [mf. BHN, SUV, NEN, SRUV, au NIV, NASB, RSV, KJV, NKJV, n.k. ikiwa utatumia Biblia ya Kiingereza], na sio Biblia iliyofafanuliwa [mf. The Living Lible, The Message ]). • Kila moduli katika mtaala wa Capstone imeainisha vitabu vya kiada ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza moduli husika. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya Capstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata orodha ya vitabu vinavyohitajika kwa ajili ya moduli hii. • Daftari na kalamu kwa ajili ya kuchukua maelezo na kufanyia kazi za darasani. • Hemphill, Ken. The Names of God . Nashville: Broadman na Holman Publishers, 2001. • Pink, A. W. The Attributes of God . Grand Rapids: Baker Book House, 1991. • Stone, Nathan. The Names of God . Chicago: Moody Press, 1944.
Vitabu na nyenzo zingine zinazohitajika
Vitabu vya kusoma
8 /
M U N G U B A B A
Muhtasari wa mfumo wa kutunuku matokeo na uzito wa gredi
Mahitaji ya Kozi
Mahudhurio na ushiriki darasani . . . . . . . 30% Mazoezi . . . . . . . . . . . . . . . . . 10% Mistari ya Kukumbuka . . . . . . . . . . . 15% Kazi za ufafanuzi wa Maandiko. . . . . . . . 15% Kazi za huduma. . . . . . . . . . . . . . 10% Usomaji na kazi za kufanyia nyumbani . . . . . 10% Mtihani wa mwisho. . . . . . . . . . . . . 10%
alama 90 alama 30 alama 45 alama 45 alama 30 alama 30
alama 30 Jumla: 100% alama 300
Mambo ya kuzingatia katika utoaji maksi
Kuhudhuria kila kipindi ni moja ya masharti ya msingi ya kozi hizi. Kukosa kipindi kutaathiri matokeo yako. Ikiwa una dharura isiyoepukika itakayokulazimu kukosa kipindi, tafadhali mjulishe mkufunzi wako mapema. Ukikosa kipindi ni jukumu lako kutafuta taarifa kuhusu kazi na mazoezi yaliyotolewa, na kuongea na mkufunzi wako pale inapobidi kufanya na kukabidhi kazi kwa kuchelewa. Sehemu kubwa ya mafunzo yanayohusiana na kozi hii hufanyika kupitia mijadala. Kwa hivyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kila kipindi kitaanza na jaribio fupi kuhusu mawazo ya msingi yaliyofundishwa katika somo lililopita. Njia nzuri zaidi ya kujiandaa na majaribio haya ni kupitia Kitabu cha Mwanafunzi na daftari uliloandikia maelezo ya somo hilo lililopita. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. Neno la Mungu ni zana yenye nguvu ambayo Mungu anaitumia ili kuwaandaa watumishi wake kwa kila kazi ya huduma aliyowaitia (2 Tim. 3:16-17). Ili kutimiza matakwa ya kozi hii, lazima uchague kifungu cha Biblia na kufanya uchambuzi wa kina (yaani, eksejesia au ufafanuzi wa Maandiko). Kazi yako iwe na kurasa tano ziliyochapwa kwa kuacha nafasi mbili kati ya mistari au kuandikwa vizuri kwa mkono, na iweze kushughulikia mojawapo ya vipengele mbalimbali vya nafsi na kazi ya Mungu Baba vilivyoangaziwa katika kozi hii. Ni shauku na matumaini yetu kwamba utashawishika kikamilifu na kuamini juu ya uwezo wa Maandiko
Mahudhurio na ushiriki darasani
Majaribio
Kukariri mistari ya Biblia
Kazi za ufafanuzi wa Maandiko
/ 9
M U N G U B A B A
kuleta badiliko na athari chanya katika maisha yako na ya wale unaowahudumia. Unapoendelea kujifunza kozi hii, uwe huru kuongeza mistari kadhaa katika uchambuzi wako (takriban mistari 4-9) kuhusu jambo ambalo ungependa kujifunza kwa kina. Maelezo yote kuhusiana na kazi hii yametolewa katika ukurasa wa 10-11, na yatajadiliwa katika sehemu ya utangulizi ya kozi hii. Matarajio yetu ni kwamba wanafunzi wote watatumia mafunzo haya kivitendo katika maisha yao na katika majukumu yao ya kihuduma. Mwanafunzi atakuwa na jukumu la kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa kutumia kanuni alizojifunza katika mazingira halisi ya huduma. Maelezo ya namna ya kufanya mafunzo kwa vitendo yanapatika katika ukurasa wa 12, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi wa kozi. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu cha Mwanafunzi ulichonacho. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” iliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi, kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. Mwishoni mwa kozi, Mkufunzi wako atakupa mtihani wa mwisho utakaofanyia nyumbani. Katika mtihani huu hautaruhusiwa kutumia vitabu vyako vya kozi hii isipokuwa Biblia. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya yale uliyojifunza katika kozi na namna yanavyoathiri mfumo wako wa fikra na utendaji wako katika huduma. Utakapokabidhiwa mtihani wa mwisho, mkufunzi wako atakupa taarifa zaidi kuhusu tarehe za kukamilisha na kukabidhi mtihani wako na kazi nyinginezo.
Kazi za huduma
Kazi za darasani na za nyumbani
Kazi za usomaji
Mtihani wa mwisho wa kufanyia nyumbani
Gredi za ufaulu
Mwishoni mwa kozi hii, gredi zifuatazo zitatolewa na kuhifadhiwa kwenye mbukumbu za kila mwanafunzi. A – Bora D – Inaridhisha B – Nzuri sana F – Hairidhishi (Feli) C – Nzuri I – Isiyokamilika
1 0 /
M U N G U B A B A
Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Zoezi hili linawakilisha sehemu muhimu ya ushiriki wako katika moduli ya Mungu Baba . Ili kutimiza takwa hili, unatakiwa uchague kifungu cha Maandiko , na ufanye utafiti na ufafanuzi wa kina ( eksejesia ) wa andiko husika. Unaweza kuchagua mojawapo ya maandiko yafuatayo: Matendo 17:24-31 Isaya 40:22-26 Warumi 9:13-18 Danieli 4:34-37 Psalms 103.9-18 Mathayo 6:25-33 Zaburi 104:24-30 Kusudi la kazi hii ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa kifungu muhimu juu ya somo la utunzaji na usimamizi wa Mungu, uhifadhi na utawala wake juu ya viumbe vyote, na maana ya hayo kwa maisha yetu leo. Pengine hakuna kitu muhimu zaidi kwa kiongozi wa Kikristo kuliko uwezo wake wa kufafanua maana ya Maandiko, na kuihusisha na masuala halisi ya maisha ya watu leo. Lengo sio tu uweze kufafanua maana ya kifungu, lakini pia kuhusisha maana hiyo moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, na maisha ya wale ambao Mungu amekuita kuwahudumia ndani na kupitia kanisa lako au huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia , ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika ? Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)
Dhumuni
Mpangilio na muundo
/ 1 1
M U N G U B A B A
2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo ? 3. Ni kitu gani Roho Mtakatifu ananiagiza kufanya kupitia kanuni hii, leo, katika maisha na huduma yangu ? Baada ya kuwa umeyajibu maswali haya katika kujifunza kwako kibinafsi, hapo sasa utakuwa tayari kuendelea kuandika ulichokigundua katika kazi uliyopewa . Angali hapa chini mfano wa muhtasari wa kazi yako: 1. Eleza kile unachoamini kuwa ndio mada kuu au wazo kuu la andiko ulilochagua. 2. Eleza kwa muhtasari maana ya andiko hilo (unaweza kufanya hivi katika aya mbili au tatu, au, ukipenda, kwa kuandika ufafanuzi mfupi wa mstari kwa mstari juu ya kifungu husika). 3. Eleza kanuni kuu moja hadi tatu au maarifa ambayo kifungu hiki kinatoa kuhusu Yesu Kristo na kazi yake. 4. Eleza jinsi kanuni moja, kadhaa, au zote zinaweza kuhusiana na yafuatayo: Kwa msaada au mwongozo, tafadhali uwe huru kusoma vitabu vya rejea vya kozi hii na/au vitabu vya mafafanuzi ( commentaries ), na kutumia maarifa yaliyomo katika vyanzo hivyo katika kazi yako. Unapotumia maarifa au mawazo ya mtu mwingine kujenga hoja zako, hakikisha unatambua kazi za waandishi husika kwa kutaja vyanzo vya taarifa hizo. Astahiliye heshima apewe heshima yake. Tumia marejeleo ya ndani ya maandishi ( in-text-refences ), tanbihi ( footnotes ), au maelezo ya mwisho ( endnotes ). Njia yoyote utakayochagua kutaja rejea zako itakubalika, ilimradi 1) utumie njia hiyo moja katika kazi nzima, na 2) uonyeshe pale unatumia mawazo ya mtu mwingine, na umtambue mwandishi husika kwa kumtaja. (Kwa maelezo zaidi, angalia katika Kiambatisho cha Namna ya Kuandika Kazi Yako: Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua Waandishi wa Vitabu vya Rejea ). Kabla hujakabidhi kazi yako, hakikisha inasifa zifuatazo: • Imeandikwa au kuchapwa vizuri na inasomeka na kueleweka. a. Kiroho chako binafsi na namna unavyotembea na Kristo b. Maisha na huduma yako katika kanisa lako la mahali pamoja c. Hali au changamoto katika jamii yako kwa ujumla.
• Ni uchambuzi wa mojawapo ya vifungu hapo juu. • Imekusanywa kwa wakati (haijacheleweshwa).
1 2 /
M U N G U B A B A
• Ina urefu wa kurasa 5. • Inafuata muhtasari au mpangilio uliotolewa hapo juu, na imeandikwa kwa namna ambayo msomaji ataweza kuelewa. • Inaonyesha jinsi kifungu husika kinavyohusiana na maisha na huduma leo. Usiruhusumaagizo haya yakuogopeshe; hii ni kazi ya kujifunza Biblia! Unachohitaji kuonyesha katika kazi hii ni kwamba ulisoma andiko husika, umeeleza kwa muhtasari maana yake, ukaweza kupata kanuni chache muhimu kutoka katika andiko hilo, na kuzihusianisha na maisha na huduma yako mwenyewe. Kazi ya ufafanuzi inabeba alama 45 na inawakilisha 15% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi yako kuwa bora na yenye maarifa ya kutosha ya Neno la Mungu. Uongozi wa Kikristo sio tu kujua kile ambacho Biblia inasema; unahusisha uwezo wa kutumia Neno la Mungu kwa njia ambayo wengine wanajengwa na kukamilishwa kwa ajili ya kazi ya huduma. Neno la Mungu ni hai na linafanya kazi, na hupenya hadi kwenye kiini cha maisha yetu na mawazo ya ndani kabisa (Ebr. 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, sio wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa na sisi kujitazama sura zetu za asili katika kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila atendalo (Yak. 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukiihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Insha ya Theolojia: Barua kwa Rafiki. Kuhudumia Neno mara nyingi huhusisha sio tu kutoa mahubiri au kufundisha darasa rasmi la Biblia, lakini kumwambia rafiki, mwanafamilia, au mfanyakazi mwenzako kwa nini unaamini kile unachoamini. Madhumuni ya insha hii ni kukusaidia kuongeza ujuzi wako katika kuzungumza kwa njia isiyo rasmi kuhusu mada muhimu za kitheolojia. Fikiria mtu unayemjua au mtu wa kufikirika anayepamba kujaribu kuelewa masuala yanayohusu Mungu na kumwamini Yesu. Mwandikie mtu huyo barua, ukieleza kwa nini imani katika Mungu ni muhimu na ina mantiki kiufahamu. Kila barua itapimwa kwa vigezo vifuatavyo: Kazi ya huduma
Utoaji maksi
Dhumuni
Mpangilio na muundo
/ 1 3
M U N G U B A B A
• Imeandikwa au kuchapwa kwa namna inayosomeka, imewasilishwa kwa wakati • Ina urefu wa kurasa mbili hadi nne • Imeandikwa kwa lugha ya kawaida ya mazungumzo ya kila siku • Hoja zimetolewa kwa uwazi na rejea za Maandiko • Ina mwaliko thabiti wa kumwamini Mungu kupitia Kristo. Insha yako inapaswa kufuatamuundowa kawaidawabarua ambayoungemwandikia rafiki. Anza barua yako na aya fupi kuhusu mlengwa wa barua hii. Toa maelezo machache kuhusu mtu huyu: umri wake, mahali anapoishi, kile anachojua kuhusu Biblia (kama kipo), uwazi wake wa sasa au wa awali kwa mjadala wa aina hiyo, n.k. Jisikie huru kufikiria aina yoyote ya mtu na hali yake ya kushughulikia. Katika sehemu ya barua yako, jenga hoja kwa rafiki yako ukimshawishi kuweka imani yake kwa Mungu. Mpe sababu, na utumie Maandiko kama msingi wa hoja na sababu hizo. Ikiwa ni lazima, fikiria juu ya vipingamizi gani anavyoweza kuwa navyo na uvijibu. Kuwa mwenye ushawishi! Zingatia, hii ni barua ya kibinafsi, sio andiko rasmi la kitaaluma. Kazi ya huduma inabeba alama 30 ambazo zinawakilisha 10% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha unashirikisha yale uliyojifunza kwa ujarisi na ripoti yako iwe yenye kueleweka vizuri.
Utoaji maksi
/ 1 5
M U N G U B A B A
Prolegomena Fundisho kuhusu Mungu na Kuenea kwa Ufalme
S O M O L A 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuyakumbuka mambo ya kwanza, prolegomena, kuhusiana na utafiti rasmi juu ya Fundisho kuhusu Mungu Baba. • Kutoa sababu za kwa nini ni muhimu sana kwa Mungu kujifunua kwetu kabla ya sisi kumjua. • Kuangazia kweli zinazohusishwa na ufunuo wa jumla, ambao ni namna ambayo Mungu hujifunua kwa watu wote kila mahali, na ufunuo maalum ambapo Mungu hujifunua kwa wanadamu maalum kwa nyakati na mahali maalum. • Kuonyesha namna Kanuni ya Imani ya Nikea inavyotoa tamko la wazi ya ukuu wa Mungu mmoja wa kweli, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. • Kutoa ushahidi wa uwepo wa Mungu (yaani, uhusika wa sasa na hai wa Mungu katika uumbaji) na umilele wake (Asili ya Mungu ya kutokuwa na ukomo na kutojulikana) • Kutoa maelezo ya maana ya sifa za Mungu, changamoto na kusudi lake, pia asili na mgawanyo wake. Warumi 1:18-20 – Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. [19] Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. [20] Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru. Kanuni ya Imani ya Nikea inaanza kwa tamko la wazi la ukuu wa Mungu mmoja wa kweli, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Inaanza na kifungu, “Tuna mwamini Mungu mmoja, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.” Huu ni uthibitisho wa ukweli ambao unatajwa kila mahali katika Maandiko: Uwepo wa Mungu unaonekana dhahiri katika adhama ya ulimwengu na uumbaji wake. Wakati ambapo jamii yetu Hakuna Udhuru Unaoruhusiwa
Malengo ya Somo
1
Ibada
1 6 /
M U N G U B A B A
hupendelea kuhoji kama ni kweli kuna Mungu au la, yaani, kama ni kweli yuko Mungu mbinguni, Biblia haijihusishi kwa namna yoyote na mjadala wa jinsi hiyo. Kinyume chake, ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu kwa sababu wamepinga kile kinachojulikana kumhusu Mungu. Sifa za Mungu zisizoonekana , zile sifa na tabia ambazo wanadamu hawawezi kuziona kwa macho ya nyama, uweza wake wa milele na asili ya kiungu, kulingana na Paulo zinafahamika wazi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Vitu ambavyo Mungu wetu mkuu ameviumba, jua na mwezi, nyota katika utukufu wake, na dunia katika fahari yake, vyote kwa pamoja vinaonyesha kwamba Mungu sio tu ni halisi, lakini pia ni mwenye uweza wote na utukufu. Mtu anawezaje kutazama ndege warukao kwa mbawa, kusikia mtoto mchanga akilia, kuona kundi la mifugo wakilishwa kwenye uwanda wa kijani unaovutia chini ya anga angavu linalong’aa, na kusema kwamba hakuna Mungu? Mtu anawezaje kupigwa na upepo mkali usoni wakati wa usiku katika msimu wa baridi, au kuona mwezi ukining’inia usiku kwa umaridadi wote katika msimu wa masika, au kuona farasi akikunjua mguu wake na kupiga hatua kamili na kuamini kabisa kwamba hakuna ufahamu wa hali ya juu nyuma ya uzuri uliotukuka wa dunia? Mpendwa rafiki, hoja yenye kushawishi zaidi kuhusu uwepo wa Mungu si ya kifundisho, ni yale yanayoonekana. Zaburi 19:1-3 - “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. 2 Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. 3 Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani.” Neno hili dhahiri la Maandiko linasisimua: mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Yaliyozungumzwa kuhusu uumbaji wa Mungu yamejitosheleza kiasi kwamba mtu yeyote mwenye akili timamu lazima akubali kwamba nyuma ya utukufu huu kuna uwepowa kiungu. Tatizo la wasioamini katika Mungu na wenye mashaka kuhusu Mungu si kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha, bali ni kwamba mioyo yao wenyewe ni migumu. Kuna uthibitisho wa kumtosha mtu kutubu; mwenye shaka hana udhuru wa kutokumjia Masihi. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Ee Mungu, ukuu wako unaijaza dunia na ulimwengu wote, lakini ulimwengu wenyewe hauwezi kukutosha, sembuse dunia, achilia mbali ulimwengu wa mawazo yangu. ~ Yves Raguin, SJ. Appleton, George, mhariri. The Oxford Book of Prayer. Oxford; New York: Oxford University Press, 1988. uk. 4
1
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
/ 1 7
M U N G U B A B A
Mungu Mwenyezi uliyeumba vitu vyote kwa wakati na nafasi na kumfanya mtu kwa sura yako mwenyewe: Utuongoze kuutambua mkono wako katika vyote ulivyoviumba na siku zote tukusifu kwa hekima na upendo wako; kwa Yesu Kristo Bwana wetu ambaye pamoja nawe na Roho Mtakatifu anatawala juu ya vitu vyote sasa na hata milele. ~ Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. Kitabu cha Mhudumu cha Kutumika Pamoja na Ekaristi Takatifu na Sala ya Asubuhi na Jioni . Braamfontein: Idara ya Uchapishaji ya Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. uk. 12
Hakuna jaribio katika somo hili
Jaribio
1
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
Hakuna maandiko ya kukariri katika somo hili
Hakuna kazi za kukusanya katika somo hili
Kazi za Kukusanya
MIFANO YA REJEA
“Kuna Mungu Mmoja Pekee – Allah.”
Unakutana barabarani na mwanachama wa Taifa la Uislam (Kundi la Waislamu Weusi linaloongozwa na Louis Farrakhan) akiuza karatasi, unasimama kwa muda mchache ili kufanya nayemazungumzo. Mnapobadili mada na kuanza kuzungumza kuhusu Mungu na Yeye ni nani hasa, kijana huyu wa kiislamu mwenye macho makali anasema kwa sauti kubwa, “Hakuna Mungu ila Allah. Yeye pekee ndiye aliyeziumba mbingu na nchi.” Je, ungejibuje madai yake?
1
“Alikuwa Wapi Wakati Huo?”
Unapozungumzia mateso ya Wayahudi walipochukuliwa utumwani na mataifa ya Ashuru na Babeli katika darasa la Shule ya Jumapili halafu mmoja wa vijana akauliza swali, “Mara zote huwa tunazungumza kuhusu Mungu kuwepo pamoja nasi, na kutupenda na kila kitu, lakini ikiwa Mungu alikuwapo pamoja na watu wake na kuwajali, kwa nini aliruhusu waumizwe na kutendewa vibaya namna hiyo? Alikuwa wapi wakati huo?” Kama mwalimu wa darasa, utajibuje swali hili muhimu la mwanafunzi huyu?
2
1 8 /
M U N G U B A B A
“Yaani Sijui.”
Mama ambaye hivi karibuni amempoteza mmoja wa watoto wake wadogo kwa ugonjwa wa saratani ya damu, amekuwa akisononeka na kuhuzunika mno. Kwa kadiri ambavyo amejaribu, anaonekana kuwa hawezi kabisa kushinda jaribu la kudhani kwamba hakuna Mungu, au, kama yupo, hawezi kuwa mwenye upendo. Kwa nini aliruhusu mtoto wao mpendwa Martha kuteseka kwa muda mrefu, na kufariki akiwa bado mdogo. Anapoendelea kufunguka zaidi anasema, “Ninapoomba, ninaposoma Biblia yangu, ninapotazama angani usiku, ninajihisi mpweke sana. Ninajua kile ninachoambiwa mara zote na mhubiri na mshauri ninayemwendea, lakini hakuna yeyote kati yao aliyenisaidia kuelewa ikiwa Mungu anatupenda, kwa nini hili lilitokea. Je, Mungu ni halisi? Je, Mungu ni mwenye upendo? Yaani, sijui.” Ungejibuje ombi la dada huyu mpendwa la kutaka kueleweshwa?
3
1
Prolegomena : Fundisho kuhusu Mungu na Kuenea kwa Ufalme Sehemu ya 1: Je, Mungu yupo, na Anajifunua Kwetu?
YALIYOMO
Mch. Dkt. Don L. Davis
Katika sehemu hii tutachunguza kusudi kuu la Mungu kujifunua kwa wanadamu kupitia ufunuo wa jumla na ufunuo maalum. Lengo letu katika sehemu hii, “ Je Mungu yupo, na Anajifunua Kwetu?” ni kukuwezesha kuona kwamba: • Prolegomena , elimu ya “mambo ya kwanza,” ya theolojia (elimu kuhusu Mungu), inayoonyesha kwamba ni lazima Mungu ajifunue kwetu ili tuweze kumjua. Hakuna awezaye kumjua Mungu bila yeye mwenyewe kujifunua kwetu. • Mungu amejifunua kwa wanadamu katika njia mbili zinazohusiana, kupitia ufunuo wa jumla na ufunuo maalum. • Kupitia ufunuo wa jumla Mungu hujifunua kwa watu wote kila mahali, na kupitia ufunuo maalum Mungu hujifunua kwa watu maalum kwa nyakati na mahali maalum.
Muhtasari wa Sehemu ya 1
/ 1 9
M U N G U B A B A
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
I. Prolegomena (inatamkwa PRAW-ley-gaw-men-uh): Kazi ya Msingi ya Elimu ya Mungu
Theolojia maana yake “elimu ya Mungu.” (“ theos ” = Mungu, “logos” = elimu ya, neno)
Yohana 17:3 “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli,
A. Ukristo hauhoji kama Mungu yupo ila unachukulia kuwa yupo na kwamba pasipo Yeye kujifunua mwenyewe, haiwezekani kumjua Mungu.
na Yesu Kristo uliyemtuma.”
1
1. Mungu jinsi alivyo katika uhalisia wake tu hajulikani, 1 Tim. 6:13-16.
a. Ni Mungu pekee ndiye awezaye kujifunua kwetu; hakuna mwanadamu awezaye kuanzisha uhusiano na Mungu.
(1) Kutoka 33:20 (2) Yohana 1:18 (3) Yohana 6:46
b. Ni Mungu pekee ndiye awezaye kutafsiri kwa usahihi maana ya ufunuo wake kwetu. (1) Yohana 1:18 (2) Mathayo 11:27
2. Mungu amechagua kujifunua kupitia kazi zake za uumbaji na ukombozi katika historia (katika uumbaji, katika ukombozi, katika Maandiko, na kwa njia ya Yesu).
a. Kwa njia ya uumbaji (1) Zaburi 19:1-3 (2) Yeremia 10:11-12
2 0 /
M U N G U B A B A
b. Kupitia historia, Mdo. 14:15-17
3. Mungu amewapa wanadamu uwezo wa kufahamu kuhusu uwepo wake, Rum. 1:18-20.
4. Ujuzi juu ya Mungu unadai uhusiano mpya na yeye kwa njia ya Yesu Kristo, na si tu elimu ya kiakili, dhana na mawazo kumhusu.
1
a. 1 Yohana 5:20
b. 2 Wakorintho 4:6
B. Umuhimu wa kujifunza kuhusu Mungu
1. Ufahamu na utafiti pekee havitoshi katika kumtambua Mungu na nafsi yake; ufahamu unahitaji kutiwa nuru na Roho Mtakatifu ili uweze kumuelewa Mungu .
2. Lazima tuzaliwe upya ili kumjua Mungu kupitia Yesu Kristo.
a. Maandalizi ya kiakili na mbinu za kisayansi pekee mara zote zitakuwa na mipaka katika tafiti za kitheolojia.
b. Ili kujifunza vizuri kuhusu Mungu, lazima umjue Mungu kibinafsi.
/ 2 1
M U N G U B A B A
3. Theolojia ni tafakari kuhusu ufunuo ; ni mawazo ya mwanadamu kuhusu nafsi ya Mungu na ufunuo wake.
a. Tunapaswa kuwa makini na namna tamaduni zetu zinavyoathiri mawazo yetu kuhusu Mungu.
b. Hatupaswi kuamini maoni yetu wenyewe kuhusu Mungu bila kusaidiwa na Roho Mtakatifu.
1
c. Kuna theolojia nyingi kwa sababu hakuna theolojia inayomwelezea Mungu kikamilifu .
d. Unyenyekevu ni sifa kuu katika kujifunza elimu ya kitheolojia.
4. Masuala ya theolojia ya kuaminika kutoka katika Maandiko na Kanisa: theolojia ni tendo la Kanisa kutafakari ufunuo wa Mungu wenye msingi wake katika Maandiko.
5. Theolojia inaweza kuingiliana na taaluma zingine lakini haipaswi kuzifuata kabisa; Ni Mungu pekee ndiye awezaye kujifunua kwetu kwa Roho wake kupitia Maandiko.
II. Mungu Mwenye Enzi Kuu Anajitambulisha Kwetu: Ufunuo wa Jumla na Ufunuo Maalum Ufunuo wa jumla: “Mungu kujitambulisha mwenyewe kwa watu wote, nyakati zote, mahali pote.” Ufunuo Maalum: “Utambulisho na udhihirisho mahususi wa Mungu mwenyewe kwa watu fulani kwa wakati fulani, utambulisho na udhihirisho ambao unapatikana sasa kwa kusoma tu maandiko fulani matakatifu [i.e., Biblia]. ” ~ Millard Erickson, Introducing Christian Doctrine, Toleo la 2. Grand Rapids: Baker Book House, 2001. uk. 42
2 2 /
M U N G U B A B A
A. Ufunuo wa Jumla: Mungu akijifunua kwa viumbe vyote kila mahali kupitia uumbaji, historia ya mwanadamu, na uwezo wa ndani wa wanadamu.
1. Mungu amejifunua kupitia uumbaji na asili .
a. Ushahidi wa Kibiblia (1) Isaya 40:25-26 (2) Warumi 1:18-20
1
(3) Matendo 14:15-17 (4) Matendo 17:24-31
b. Hoja za kifalsafa kuhusu theolojia ya asili: Thomas Aquinas (1) Uthibitisho wa kikosmolojia : Mungu kama sababu ya kwanza isiyosababishwa (2) Uthibitisho wa kiteleolojia : Mungu ndiye mwanzilishi mkuu wa utaratibu na makusudi ya ulimwengu. (3) Hoja za kianthropolojia : Utaratibu wa kimaadili unathibitisha kwamba kuna Mungu na atahukumu matendo yetu. (4) Hoja za kiontolojia (Anselm): Zaidi ya vyenye uhai vyote vinavyoweza kufikirika Mungu ndiye mkuu.
2. Mungu amejifunua katika historia ya mwanadamu .
a. Kuhifadhiwa kwa watu maalum wa Mungu, Israeli.
b. Kazi ya ukombozi wa Mungu katika historia ya mwanadamu: Yesu wa historia, Mdo. 2:22-23 (1) Historie: historia halisi ya mwanadamu
/ 2 3
M U N G U B A B A
(2) Heilsgeschicte: Kazi ya Mungu ya kihistoria katika taifa la Israeli hadi kufikia kwa Yesu Kristo.
3. Mungu amejifunua ndani ya wanadamu wenyewe.
a. Ufahamu, Isa. 1:18
b. Maamuzi ya kimaadili: dhamiri, Rum. 2:15
1
c. Asili ya kidini: tamaduni zote za kibinadamu hubeba dhana fulani ya kimungu.
(1) Zaburi 10:4 (2) Zaburi 73:3
B. Ufunuo maalum: tendo la Mungu kujifunua kwa watu fulani, wakati na mahali fulani.
1. Ufunuo maalum ni wa kibinafsi (Mungu anajifunua mwenyewe kwetu).
a. Mimi niko, Ambaye niko, Kut. 3:14-15.
b. Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo (1) Kutoka 3:6 (2) Kutoka 4:5
2 4 /
M U N G U B A B A
2. Ufunuo maalum unahusiana na wanadamu [anthropic] (anthropology = “anthropos,” mwanadamu, “logos,” elimu ya): Mungu hutumia lugha na maumbo ya kibinadamu kuwasiliana nasi.
a. Katika ulimwengu wa lugha na uzoefu wa mwanadamu, 1 Kor. 2:12-13.
b. Katika nafsi ya Yesu Kristo. (1) Yohana 1:14 (2) Yohana 1:18 (3) Luka 10:22
1
3. Ufunuo maalum ni wa [kianalojia] kimifano . (Mungu hutumia mifano ili kutuonyesha yeye ni nani na jinsi uhusiano wetu na yeye ulivyo).
a. Mfano = hutusaidia kulielewa jambo moja kwa kulilinganisha na jambo lingine: kama A ilivyo kwa B, ndivyo C ilivyo kwa D. (1) Yohana 10:9 (2) Yohana 10:14-15
b. Mungu ndiye huchagua vitu vya kulinganisha, na huelezea uhusiano baina ya vitu hivyo kwa ajili ya uelewa wetu.
c. Yeye huwasiliana na mtu katika ujumla wake, si tu kwa dhana au mawazo pekee (mf., Yesu ni Simba wa Yuda).
4. Ufunuo maalum ni halisi.
/ 2 5
M U N G U B A B A
a. Kupitia matukio ya kihistoria (mf., wito wa Ibrahim), Mwa. 12:1-3
b. Kupitia hotuba za kiungu, mf., Ebr. 1:1-2
c. Kupitia kufanyika mwili kwa Yesu Kristo, 1 Yohana 1:1-3
Hitimisho
1
» Ili tumfahamu Mungu ni lazima Yeye mwenyewe ajifunue kwetu.
» Mungu hujifunua kwetu katika namna au njia mbili maalum: kupitia ufunuo wa jumla, Mungu hujifunua kwa watu wote kila mahali, na kupitia ufunuo maalum, Mungu hujifunua kwa watu fulani, wakati na mahali fulani.
Tafadhali tumia muda mwingi kadiri uwezavyo kujibu maswali haya na mengineyo ambayo huenda umeyapata kutokana na video. Umuhimu wa Mungu kujifunua kwetu, na asili ya ufunuo wa jumla na ufunuo maalum ndio kiini hasa cha somo letu la Mungu Baba. Majibu yawe ya wazi na kwa kifupi, na ikibidi, tumia Maandiko kuunga mkono majibu yako! 1. Nini maana ya neno “ prolegomena ”? Kwa nini ni muhimu kupambanua nadharia ulizonazo kwanza kabla ya kujihusisha na elimu rasmi kuhusu Mungu na kazi yake? 2. Kwa nini haiwezekani mtu kumjua Mungu kwa namna zake na nguvu zake mwenyewe? 3. Je, ufahamu na utafiti vina nafasi gani katika kujifunza kuhusu Mungu? Na kwa nini havitoshi katika kumsaidia mtu yeyote kupata ujuzi kamili wa Mungu? 4. Roho Mtakatifu ana wajibu gani katika kutusaidia kumjua Mungu? 5. Je, ufunuo wa jumla ni nini ? Ni kwa njia zipi mahususi Mungu amejifunua kwa wanadamu wote kila mahali? Je, ufahamu kuhusu Mungu unatosha kuokoa? Elezea zaidi jibu lako.
Sehemu ya 1
Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
2 6 /
M U N G U B A B A
6. Je, ufunuo maalum ni nini? Zipi ni sifa za ufunuo maalum? Ni njia ipi ya wazi na yenye nguvu zaidi ambayo Mungu amewahi kujifunua kwa wanadamu? 7. Kwa nini ni muhimu Mungu mwenyewe kujifunua kwetu, iwe ni kupitia ufunuo wa jumla au maalum? Ni upi basi, unapaswa kuwa mtazamo wetu kila mara tunapojifunza kuhusu Mungu?
Prolegomena: Fundisho kuhusu Mungu na Kuenea kwa Ufalme Sehemu ya 2: Je, Mungu Anaweza Kujulikana Kwetu?
1
Mch. Dkt. Don L. Davis
Kama Mungu aliyeziumba mbingu na nchi, Baba yuko na anafanya kazi kila mahali katika ulimwengu (yaani, Mungu yupo kati yetu – “immanent” ) , na vilevile zaidi ya uumbaji na viumbe vyote yeye hana kikomo (yaani, Mungu yuko juu ya fahamu – “transcendent”). Katika theolojia, tunasoma sifa za Mungu , sifa zile zinazoelezea tabia mbalimbali za ukuu na wema wa milele wa Mungu. Lengo letu katika sehemu hii, “Je, Mungu Anaweza Kujulikana kwetu?” ni kukuwezesha kuona kwamba: • Mungu, kama Muumba na aliyefanya vitu vyote, anao uhusiano wa kipekee na ulimwengu wake, uhusiano unaoweza kuelezewa kwa misingi ya uwepo wake katika uumbaji wake [yaani immanence] na sifa yake ya kuwa juu ya fahamu [yaani transcendence] . • Uwepo wa Mungu katika uumbaji wake unarejelea uhusika wake wa sasa na hai katika uumbaji wake wote. • Kwa upande mwingine, sifa yake kama Aliye juu ya fahamau [transcendence] inarejelea asili yake ya kutokuwa na kikomo na kule kutojulikana kwake. • Sifa za Mungu ni sifa na tabia za Utatu Mtakatifu – Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. • Tunaweza kuzigawanya sifa za Mungu kwa misingi ya ukuu wake na wema wake.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
/ 2 7
M U N G U B A B A
• Sifa zinazohusiana na ukuu wa Mungu ni hali yake ya kiroho, uzima wake, haiba yake, kutokuwa na kikomo, na kudumu kwake. • Sifa zinazohusiana na wema wa Mungu zinahusisha utakatifu, ukamilifu, uadilifu, na upendo.
I. Uwepo wa Mungu katika Uumbaji wake na Sifa yake ya Kuwa Juu ya Fahamu
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
1
A. Fafanuzi: jozi hii ya mkazo inahusiana sana na uhusiano wa Mungu na uumbaji wake kama Muumba wa mbingu na nchi, na wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Kanuni ya Imani ya Nikea, ambayo inatumika kama msingi wa kitheolojia wa mtaala wetu, inaanza na tamko la wazi la ukuu wa Mungu mmoja na wa kweli, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Inaanza na kifungu, Muumba wa mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.” Tamako hili linasisitiza vyote: uwepo wa Mungu katika uumbaji wake na sifa yake ya kuwa juu ya fahamu. “Tuna mwamini Mungu mmoja, Baba Mwenyezi,
1. Uwepo wa Mungu katika Uumbaji = Mungu yupo na anatenda kazi kila mahali ndani ya ulimwengu.
2. Sifa ya Mungu ya Kuwa Juu ya Fahamu = Nafsi ya Mungu ipo juu zaidi ya uumbaji na uwezo wa chenye uhai chochote kujielewa isipokuwa yeye mwenyewe.
B. Uwepo wa Mungu katika Uumbaji
1. Mungu yupo na anatenda kazi katika uumbaji.
a. Yeremia 23:23-24
b. Zaburi 135:5-7
2. Mungu yupo na anatenda kazi katika jamii ya wanadamu.
2 8 /
M U N G U B A B A
a. Zabruri 139:1-10
b. Danieli 4:35
3. Umuhimu wa Uwepo wa Mungu katika Uumbaji
a. Mungu anaweza kutumia njia zinazofikika kwa ujumla na za ulimwengu wote kufanya mapenzi yake ulimwenguni.
1
b. Mungu yuko huru kutumia chochote na mtu yeyote kutimiza mapenzi yake.
c. Uumbaji wote wa Mungu unadhihirisha utukufu wake na kazi ya mikono yake.
d. Uumbaji huwapa wanadamu (katika kiwango kimoja) maarifa ya kweli ya Mungu.
e. Kuna namna fulani ya maelewano baina na kati ya watu wote kwa sababu Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote.
C. Sifa ya Mungu Juu ya Uumbaji
1. Mungu yuko juu na zaidi ya vitu vyote alivyoumba: vimetokea kwa njia yake na kwa utukufu wake pekee.
a. 1 Wafalme 8:27
b. 2 Nyakati 6:18
/ 2 9
M U N G U B A B A
c. Nehemia 9:6
d. Isaya 66:1
2. Mungu hawezi kujulikana kupitia jitihada na shughuli za wanadamu; utukufu na asili yake ni zaidi ya upeo wa ufahamu na uzoefu wa mwanadamu.
1
a. Kumbukumbu 10:14
b. Zabruri 113:4-6
3. Matokeo ya Sifa ya Mungu kuwa Juu Zaidi ya Vyote
a. Uzima wa mwanadamu sio na wala haujawahi kuwa aina ya uzima wa hali ya juu zaidi katika ulimwengu.
b. Mungu hawezi kuwekewa mipaka au kushikiliwa na dhana ambazo theolojia au taaluma nyingine zozote hutengeneza kumhusu.
c. Ni Mungu pekee ndiye avirudishaye vitu vyote chini ya utawala wake kwa ajili ya wokovu wetu na hatimaye kwa utukufu wake mwenyewe.
d. Mungu ni wa namna yake, sui generis (i.e., yupo katika kundi la peke yake). Hakuna kiumbe mwingine anayeweza kuufikia utukufu wake.
e. Mungu ni wa kuogopwa zaidi ya vyote na kuliko kila kitu.
3 0 /
M U N G U B A B A
f. Tunapaswa kutarajia Mungu kuwa na kutenda zaidi yetu na zaidi ya mawazo yetu katika kila jambo.
II. Changamoto Tunayokutana nayo katika Kujifunza Kuhusu Mungu: Tatizo na Kusudi katika Kujifunza Sifa za Mungu.
A. Umoja wa Mungu na sifa za Mungu
1
1. Ufafanuzi wa sifa za Mungu = “zile tabia za Mungu zinazohusisha vile alivyo. Ndizo sifa zenyewe hasa za asili yake.” Erickson, Introducing Christian Doctrine, uk. 89.
2. Asili ya Mungu mmoja aliye katika utatu ni jumuishi na kamili.
a. Asili ya Mungu (kwa ajili ya kujifunza tu) inaweza kutenganishwa kwa ajili ya uchambuzi na ibada.
b. Hata hivyo, Mungu mwenyewe ni nafsi kamili ambaye hutumia kila sifa kwa uwiano na upatano mkamilifu na sifa nyingine zote kwa umoja na kwa ukamilifu wa mapenzi yake na nafsi yake katika kila tendo.
3. Changamoto: Je, tunaweza kweli kuelewa tabia nzima ya Mungu kwa kuchanganua tu sifa zake mahususi?
a. Mungu ni mmoja.
(1) Kumbukumbu 6:4 (2) Kumbukumbu 4:35
(3) Isaya 42:8 (4) Isaya 44:6
/ 3 1
M U N G U B A B A
(5) Isaya 44:8 (6) Yeremia 10:10
b. Sifa za Mungu zote zimefungamanishwa.
c. Hakuna mtu yeyote awezaye kufanya uchambuzi wa nafsi ya Mungu.
1
d. Kuna namna tunapungukiwa katika uchunguzi wetu kuhusu Mungu (tuna kawaida ya kukazia tabia moja huku tukizitenga au kuziacha nyinginezo).
4. Njia za kuondokana na tatizo hilo
a. Kuwa makini katika maoni na mitazamo yako.
b. Kuwa na ufahamu wa uwepo wa tabia ya kupunguza.
c. Kuwa mnyenyekevu katika matamko yako kuhusu Mungu.
B. Kusudi la somo la sifa za Mungu
1. Kutafakari ukamilifu wa Mungu kwa uhakika na kwa ujasiri, Zab. 40:4-5.
2. Kuwaza mawazo ya Mungu kama yeye awazavyo hasa katika msingi wa uweza wake, Yohana 14:26.
3 2 /
M U N G U B A B A
3. Kujifunza kuhusu utukufu wa Mungu uliofunuliwa katika uumbaji na katika Yesu Kristo.
a. Yohana 17:3
Wajibu mzito kabisa ulio juu ya kanisa la Kristo leo ni kutakasa na kuinua dhana yake kuhusu Mungu hadi dhana hiyo itakapoonekana tena kumstahili Mungu na kanisa. Katika sala na kazi zake zote hili linapaswa kuwa la kwanza. Tunakitendea haki zaidi kizazi kijacho cha Wakristo kwa kuwarithisha, bila kufifishwa na bila kupunguza, dhana hiyo adhimu ya Mungu ambayo tumeipokea kwa baba zetu Waebrania na Wakristo wa vizazi vilivyopita. Hili litathibitika kuwa la thamani zaidi kwao kuliko kitu chochote ambacho sanaa au sayansi inaweza kubuni. ~ A.W. Tozer. The Knowledge of the Holy. New York: Harper San Francisco, 1961. uk. 4.
b. Mathayo 11:25-27
4. Kumfanya Mungu ajulikane kwa wengine, Zab. 71:17-19
1
III. Muundo wa Somo la Mungu: Asili na Mgawanyo wa Sifa za Mungu
A. Asili ya sifa za Mungu
1. Sifa zinazoakisi tabia za utatu wa Mungu wote.
a. Si sawa na tabia, yaani, kazi zile ambazo zinahusiana na kila nafsi katika Utatu.
b. Si sawa na shughuli au matendo ya washiriki wa utatu, ambayo ni sifa mahususi za kila nafsi katika Utatu.
2. Sifa hizi ni tabia za kudumu, ambazo ni za Mungu kwa asili.
3. Sifa huzungumza juu ya kiini hasa cha Mungu alivyo.
/ 3 3
M U N G U B A B A
B. Mgawanyo wa sifa za Mungu
1. Ukuu wa Mungu (ni jumla ya tabia zinazohusiana na utukufu wa Mungu, Mungu katika Uungu wake, mara zote katika kazi za kitheolojia huitwa “sifa za asili”)
a. Hali yake ya kiroho
1
b. Uzima wake
c. Haiba
d. Kutokuwa na kikomo
e. Kudumu kwake
2. Wema wa Mungu (jumla ya tabia zinazohusiana na uhusiano wa Mungu na uumbaji wake, ikiwemo wanadamu, mara zote katika kazi za kitheolojia huitwa “sifa za kimaadili”)
a. Utakatifu
b. Uadilifu/ukamilifu
c. Upendo
3 4 /
M U N G U B A B A
Hitimisho
» Kama aliyefanya na kuumba vitu vyote, Mungu anahusiana na ulimwengu wake kama aliyeko katika uumbaji wake na ambaye yuko juu sana ya uumbaji. » Kama aliyeko katika uumbaji, Mungu yuko na anahusika kikamilifu katika ulimwengu. » Kama aliye wa juu ya uumbaji , Mungu hana kikomo na hawezi kujulikana pasipo kutuwezesha kumuona na kumjua.
» Sifa za Mungu zinarejelea tabia za ukuu na wema wake.
1
Maswali yafuatayo yaliundwa maalum kukusaidia kufanya mapitio ya maarifa yaliyomo katika sehemu ya pili ya video. Kama Kanuni ya Imani ya Nikea inavyodokeza, kuna Mungu mmoja tu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Kama aliyepo na anayefanya kazi katika uumbaji wake, lakini pia aliye juu zaidi ya uumbaji wake, lazima tuelewe sifa zake kwa kuzingatia ukuu na wema wake. Unapotafakari juu ya maswali yaliyo hapa chini, majibu yako yawe rahisi na ya moja kwa moja, na inapobidi, yaunge mkono kwa Maandiko! 1. Kanuni ya Imani ya Nikea inadokeza kwamba Baba Mwenyezi ndiye Muumba wa mbingu na nchi, wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Kwa nini unafikiri huu ni ukweli wa kwanza na wa msingi kwa majadiliano yote na kujifunza juu ya Mungu? Elezea jibu lako. 2. Ipi ni asili ya uwepo wa Mungu katika uumbaji [immanence]? Ni kwa namna zipi Mungu hutuonyesha kuwa yupo na anajihusisha kikamilifu na mambo ya uumbaji na wanadamu? 3. Kwa nini ufahamu wa uwepo wa Mungu katika uumbaji ni wa muhimu sana kwetu kama wanafunzi wa theolojia? Je, zipi zinaweza kuwa athari za fundisho hili kwa umisheni, kwa ajili ya kuwavuta watu ambao hawana maarifa ya Mungu katika Yesu Kristo? 4. Ipi ni asili ya sifa ya Mungu kuwa juu zaidi ya uumbaji [transcedence]? Kwa nini ni lazima tusisitize kwamba Mungu hawezi kujulikana jinsi alivyo na kuhusu alivyo bila msaada wa Roho Mtakatifu?
Sehemu ya 2
Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
/ 3 5
M U N G U B A B A
5. Yapi ni matokeo ya kumuelewa Mungu kama aliye juu ya vitu vyote? Ni kwa namna gani fundisho hili linaweka msingi kwa ibada na utumishi wote halali kwa Mungu? 6. Je, sifa ya Mungu ni nini ? Kwa nini ni muhimu mara zote kukumbuka umoja wa Mungu tunapojifunza sifa zake za kibinafsi? Ni makosa gani ambayo ni lazima tuyaepuke tunapotafuta kuelewa sifa za Mungu moja baada ya nyingine, nje ya sifa nyingie zote alizonazo? 7. Ni kwa namna gani wanatheolojia huzigawa sifa za Mungu katika makundi? Ni sifa zipi zinahusiana na ukuu wa Mungu, na sifa zipi zinahusiana na wema wa Mungu? Somo hili linaangazia zile kweli muhimu, za kwanza ambazo tunapaswa kuzifahamu kwa ajili ya mafunzo thabiti ya kibiblia kuhusu Mungu. Ni muhimu sana mtu kupata “picha kubwa” ya mchakato wake wa kujifunza kabla ya kuchimbua mambo mazito yanayohusu nafsi na kazi za Mungu. Tukijua dhana iliyo nyuma ya somo letu, tutaongozwa katika kweli ya Fundisho kuhusu Mungu. Katika kila hatua ni lazima tujilinde dhidi ya kiburi na majivuno, na kujidhania kwamba tunaweza kuielewa nafsi ya Mungu pasipo kusaidiwa na Roho Mtakatifu, na bila Yeye mwenyewe kuyaangazia Maandiko. Yafuatayo ni baadhi ya mawazo muhimu tuliyoshughulika nayo katika kujifunza kwetu somo la kwanza. ³ Prolegomena, elimu ya “mambo ya kwanza” ya Fundisho la Mungu, ni muhimu kwa elimu halali, ya kibiblia kuhusu Fundisho la Mungu Baba, au theolojia kamili. ³ Kwa sababu ya asili ya Mungu na hali yetu ya kuwa na ukomo, ni lazima tuweke wazi kwamba ni lazima Mungu ajifunue kwetu ndipo tuweza kumfahamu. ³ Tunapojua kuwa Mungu ni zaidi ya fahamu na tafakari zetu, ni lazima tuwe wanyenyekevu na waangalifu katika tafakari na madai yetu yote kuhusu Mungu na nafsi yake. Ili tumjue Mungu kibinafsi ni lazima ajifunue yeye mwenyewe kwetu. ³ Kama Muumba wa vitu vyote, Mungu amejifunua kwetu katika namna mbili maalum. Katika ufunuo wa jumla, Mungu amejifunua kwa watu wote kila mahali, na katika ufunuo maalum, Mungu hujifunua kwa watu fulani kwa wakati na mahali fulani.
1
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Muhimu
Made with FlippingBook - Online catalogs