Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

1 0 8 /

M U N G U B A B A

MAZOEZI

Mathayo 3:16-17

Kukariri Maandiko

Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/books kupata kazi ya kusoma ya juma lijalo, au muulize mkufunzi wako.

Kazi ya Usomaji

Tafadhali kabidhi kwa mwalimu wako karatasi yako ya kazi ya usomaji iliyo na muhtasari wako wa kazi za usomaji za wiki. Kadhalika, hakikisha kwamba umechagua kifungu chako chaBiblia kwa ajili ya kazi yako ya eksejesia, na uhakikishe pia kwamba unaelewa vigezo na tarehe za kukamilisha kazi yako. Neno kwa wenye hekima: ni bora kujipanga mapema na kuwa mbele ya ratiba kuliko kulazimishwa kufanya kazi ya kukariri katika dakika za mwisho. Zungumza na Mshauri wako, na hakikisha unazo taarifa zote muhimu, na umekabidhi mapendekezo yako mapema iwezekanavyo ili uwe na muda mwingi na uanze kukamilisha kazi hizi kwa wakati. Somo letu la mwisho litajikita katika sifa za Wema wa Mungu . Wema wa ajabu wa Mungu unaonyeshwa katika sifa zake za kiadili za usafi, ukamilifu, na upendo usio na mipaka. Kuhusiana na usafi wake mkamilifu wa kiadili, tutachambua utakatifu, uadilifu, na haki yake. Kuhusiana na ukamilifu wake tutachunguza uhalisi, ukweli, na uaminifu wake. Hatimaye, kuhusiana na upendo wake, tutaangazia ukarimu wake, neema, rehema, na ustahimilivu wake. Pia tutachunguza kwa pamoja uhusiano kati ya wema wa Mungu na ukali wake, tukichunguza ghadhabu ya Mungu na uhusiano wake na upendo wake wa ajabu.

Kazi Nyingine

3

Kuelekea Somo Linalofuata

Made with FlippingBook - Online catalogs