Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 1 1 5

M U N G U B A B A

Mungu kama Baba: Wema wa Mungu Sehemu ya 1: Sifa za Kiadili za Wema

YALIYOMO

Mch. Dkt. Don L. Davis

Mungu huonyesha wema wake kupitia sifa zake za kiadili za usafi, ukamilifu, na upendo kamili usio na mipaka. Anaonyesha usafi wake kamili kupitia utakatifu, uadilifu, na haki yake. Huonyesha ukamilifu wake kupitia sifa zake za uhalisia, ukweli, na uaminifu. Mwisho kabisa, Mungu hulionyesha pendo lake lisilo na mipaka kupitia sifa zake za ukarimu, neema, rehema, na ustahimilivu wake. Lengo letu katika sehemu hii, Sifa za Kiadili za Wema, ni kukuwezesha kuona kwamba: • Wema wa ajabu wa Mungu unaoonyeshwa katika sifa zake za kiadili za usafi, ukamilifu, na upendo wake kamili usio na mipaka. • Usafi kamili wa Mungu unaonyeshwa kupitia utakatifu, uadilifu, na haki yake. • Mungu Baba Mwenyezi pia huonyesha wema wake kupitia sifa zinazohusiana na ukamilifu wake, yaani uhalisia, ukweli, na uaminifu wake. • Upendo wa Mungu, kama kielelezo cha wema wake wa kiungu, unahusishwa na sifa zake za ukarimu, neema, rehema, na ustahimilivu. • Kuelewa wema wa Mungu hutuongezea ujasiri na uhakika wa kumwamini na kumtumikia Mungu wetu mpendwa asiye na mwisho.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

4

I. Mungu Baba Mwenyezi Ana Usafi wa Kiadili Mkamilifu.

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

Wanatheolojia wanaurejelea usafi wa kiadili wa Mungu kama utakatifu wake kamili, uzuri kamili unaoonyeshwa katika kujitenga kwake na kuwa huru na chochote kibaya, cha dhambi, uharibifu, au kiovu. Ukamilifu huo kamili wa kiadili unafunuliwa katika utakatifu, uadilifu, na haki yake.

Made with FlippingBook - Online catalogs