Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 1 4 1

M U N G U B A B A

³ Wema wa Mungu Baba Mwenyezi unadhihirishwa katika sifa zake za kiadili za usafi, uadilifu, ukamilifu, na upendo kamili usio na mipaka. ³ Usafi wa kiadili wa Baba unadhihirishwa kupitia utakatifu, haki na hukumu za haki. ³ Uadilifu na ukamilifu wa Mungu unahusishwa na sifa za uhalisi wake, ukweli na uaminifu. ³ Upendo wa Mungu Baba unaonyeshwa kupitia sifa za ukarimu, neema, rehema, na ustahimilivu wake (uvumilivu na subira). ³ Ghadhabu ya Mungu ni moja ya mafundisho makuu na ya msingi katika Neno la Mungu, na namna yoyote ya kulipuuza lazima itaharibu taswira ya jumla ambayo mtu anayo kwa habari ya utukufu wa Mungu. ³ Mungu huonyesha ghadhabu yake katika kitendo anachofanya kama kisasi dhidi ya wale wanaompinga yeye na mapenzi yake mema. ³ Ghadhabu yaMungu kamwe haielekezwi mahali kwa namna ya kimihemko, isiyo na haki, au kiholela bila kufikiri. Siku zote hutolewa kwa usahihi na inahusishwa na hasira yake ya haki dhidi ya mambo yale yote yanayopinga utawala na mapenzi yake. ³ Ghadhabu ya Mungu, kama sifa ya kiadili ambayo mara zote inahusishwa na ukali wa Mungu na si wema wake, ili ieleweke na kupewa heshima stahiki ni lazima itazamwe katika mwangaza wa wema wa Mungu. Upendo na haki ni lazima vieleweke kwa pamoja. ³ Mvutano wowote tunaoweza kuuona kati ya utakatifu wa Mungu na upendo wake si mvutano halisi ndani ya Mungu, bali ni shida katika tafakari za fahamu zetu zenye mipaka kuhusiana na sifa kamili za Mungu na asili yake. ³ Hakuna mkanganyiko au mvutano uliopo kati ya sifa za Mungu katika asili yake na jinsi alivyo. ³ Kila mahali Mungu anapotenda na kufanya kazi, yeye ni Mungu mmoja wa kweli na atadumu milele katika sifa hiyo, daima akitenda kila mahali kwa upatanifu kamili wa upendo na haki yake, neema na kweli yake.

4

Made with FlippingBook - Online catalogs